- Kilimo

Kilimo cha mbogamboga chatia chachu kwa maendeleo ya elimu

Sambaza chapisho hili

Wakati Tanzania ikikabiliwa na changamoto katika kuhakikisha lishe bora kwa watoto hasa katika maeneo ya vijijini na mijini, kuanzishwa kwa kilimo cha mbogambogambogamboga katika shule za msingi kunaweza kuwa ni kichocheo cha mabadiliko ya namna bora ya kujenga na kuelimisha akili changa za vijana na kuwafanya wakue katika mazingira bora ya kufikiri na kudadisi mambo mbali mbali.

Haya yanaweza kushuhudia na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Losikito Bwana Enea Loshaisho ambapo amesema ”walimu wa shule wameshuhudia mara kwa mara wanafunzi wengi wakifika shuleni na kushinda mchana kutwa wakiwa na njaa hali ambayo ilikuwa ikichangia kuporomoka kwa ufaulu na umakini wa wanafunzi shuleni. Hivyo mbinu mbadala zilihitajika ikiwemo kuhakikisha chakula cha mchana kina nyongeza ya mbogambogambogamboga ili kuwapatia lishe kamili. Hata hivyo mlo ambao wanafunzi wamekua wanapata ni mlo wa wanga tu kupitia chakula cha makande”.

Kupitia wadau wa kilimo Ikolojia na utayari wa shule za msingi ili kuleta mabadiliko katika mlo kwa shuleni za msingi za mkoa wa Arusha ziliamua kuchukua hatua na kufanya uzalishaji wa mbogambogambogamboga kwa vitendo. Kwa pamoja, waliamua kutoa eneo la shule ili kuweka miundo mbinu muhimu kama vile uvunaji wa maji ya mvua, mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone pamoja na kuandaa shamba la kupanda mbogamboga mbogamboga na matunda.

Miundo mbinu hii ya uanzishaji wa bustani ililenga kuhakikisha kuwa maji yanapatikana wakati wote wa mwaka na mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone ulilenga kuongeza ufanisi katika matumizi ya maji hivyo kuifanya ardhi iwe na uzalishaji mzuri wa mbogamboga na matunda. Wanafunzi pamoja na walimu sasa walipata kujifunza jinsi ya kuandaa ardhi, kupanda mbegu, na kutunza mimea hadi kuvuna. Hii siyo tu iliwapa wanafunzi ujuzi wa kilimo, bali pia iliwapatia nafasi ya kujifunza stadi za maisha na kufanya kazi kwa pamoja.

Hata hivyo ndani ya miezi michache, shule imekuwa ikivuna mbogamboga za kutosha kwa ajili ya chakula cha mchana cha wanafunzi. Na hivi sasa, badala ya kula mlo wenye vyakula vya wanga tu, wanafunzi wanafurahia milo yenye mbogamboga safi zenye virutubisho vingi. Hii inaboresha afya zao na kuwafanya wawe na utayari na umakini darasani.

Kupitia kilimo, wanafunzi wamejifunza uzalishaji wa mbogambogambogamboga na matunda kwa vitendo, umuhimu wa lishe bora, makundi matano ya vyakula na jinsi ya kuchangia katika ustawi wa jamii yao. Wanafunzi wanayofuraha kuona matunda ya kazi zao na hii inawaongezea motisha ya kuja shuleni kila siku. Walimu pia wameona mabadiliko makubwa kwani wanafunzi wamekuwa na shauku ya kujifunza zaidi kuhusu kilimo cha mbogamboga mbogamboga.

Mafanikio haya yameweza kubadili mtazamo wa eneo lisilo la uzalishaji kuwa sehemu ya kujifunzia kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Shamba la shule sasa limekuwa darasa la wazi, ambapo wanafunzi wanajifunza kuhusu kilimo endelevu, umuhimu wa mazingira, na jinsi ya kujitegemea kwa chakula. Jamii pia inashiriki katika shughuli hizi, ikijifunza mbinu bora za kilimo na umuhimu wa lishe bora.

Moja ya wanafunzi wa kidato cha sita Gift Meinyal anasema, “Ninapenda sana kushiriki katika shamba la shule kwa sababu ninajifunza mengi kuhusu kilimo ikiwemo kuzalisha Chakula bora cha mbogamboga mbogamboga bila kutumia dawa na mbolea za viwandani”.

Uanzilishaji wa bustani za mbogamboga mbogamboga umekuwa na mapokeo chanya katika jamii, hasa baada ya hamasa iliyoletwa na bustani za shule kwani zimeweza kuhakikisha kuna upatikanaji wa chakula safi na salama shuleni, kumepunguza pia gharama za chakula na kusaidia kuinua elimu ya kujitegemea kupitia shughuli za kilimo wanazofanya wanafunzi muda wa ziada wakiwa shuleni.

Wananchi wameanza kuelewa thamani na kuiga kuwa na bustani za mbogamboga mbogamboga na sasa familia nyingi zimeanza kuiga mfano huo kwa kuanzisha bustani ndogondogo katika maeneo ya nyumba zao huku wanafunzi wakitumia ujuzi wanaoupata shuleni kwa kuwafundisha ndugu na marafiki wanaporudi majumbani. Hii imekuwa fursa nzuri ya kuboresha afya, kuongeza kipato na kusaidia kujenga ustawi wa kijamii nzima.

Kutokana na mafanikio haya ni wakati mwafaka sasa kwa Watanzania wote kuhamasika na kuanza kulima mbogamboga mbogamboga katika maeneo ya nyumba zao. Hii ni hatua muhimu sio tu kwa kuboresha afya na lishe, bali pia kwa kujenga uwezo wa kujitegemea katika upatikanaji wa chakula. Aidha, kilimo hiki kidogo kinaweza kuwa chanzo cha mapato ya ziada, kusaidia kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa kaya kwa wote waishio mijini na vijijini.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *