Wakulima wanalalamika kwamba hawawezi kupata soko ya mazao yao. Katika dunia ya sasa, teknolojia ya habari na masawasiliano, uboreshaji wa miundo msingi ya usafiri na uchukuzi, ikiwemo barabara, soko imeanza kubadilika kuliko awali. Soko imeanza kuwa wazi na yenye ushindani mkubwa, na hii inatoa fursa kwa wakulima wadogo, hasa wale wa kilimo hai ambao wana uwezo wa kutumia mtandao, yaani intaneti (Mtandao wa mawasiliano ya kimataifa ya kikompyuta).
Kwa kiasi kikubwa, kilimo cha sasa inaongozwa na mahitaji ya mnunuzi au mtumiaji wa mazao na bidhaa ya kilimo. Hivyo, maswali haya yatamwelekeza mkulima katika kufanya uamuzi wa zao la kuzalisha: Mnunuzi ni nani? Anapatikana wapi? Ninaweza kumfikia kwa njia gani au ni nani anaweza kumfikia mnunuzi kwa niaba yangu?
Mkulima lazima afikiria soko; kuanzia shambani hadi sahani ya mlaji. Mkulima sio mzalishaji tu, bali pia ni muuzaji. Kujua misimu na mabadiliko yanayoendelea sokoni itampa mkulima uwezo wa kufanya maamuzi mwafaka katika shughuli zake za uzalishaji, atafikia soko na wanunuzi, na bei ya bidhaa.
Miji yanayokua yanatoa fursa ya soko ya uhakika na wakulima wanaoishi na kuzalisha karibu na miji hayo wana nafasi kubwa ya kuuza na kupanua kilimo. Miji mikubwa ya Tanzania kama vile Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na mengine yana mamilioni ya wakaaji ambao wanatumia mazao kutoka kwa wakulima kila siku. Watu hawa wanakula nini? Kuzalisha kukidhi mahitaji ya chakula vikundi tofauti ya wakaazi hawa ni fursa kubwa kwa wakulima wadogo.