Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara wanayoleta kwenye mimea. Iwapo mandhari hayatakua na uwiano basi sehemu moja inaweza kuwa na idadi kubwa ya wadudu waharibifu hivyo kusababisha madhara.
Madhumuni ya njia hizi za asili ni kujaribu kuweka uwiano katika mazingira. Mfumo huu haukusudii kuangamiza wadudu bali kuwakabili.
Ni bora basi kuchukua tahadhari na kuzuia mimea isishambuliwe ili kudhibiti hasara inayoweza kupatikana iwapo mimea itashambuliwa (sio mazao hafifu, bali pia gharama kubwa ya madawa).
Je, kutumia njia za kiasili ni bora kuliko madawa ya kemikali?
Madawa ya kemikali hayajaleta suluhisho na ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la magonjwa na wadudu katika mimea. Matumizi ya kemikali yameongezeka zaidi kipindi cha miaka 50 iliyopita ilihali idadi ya magonjwa na wadudu imezidi kuongezeka na wengine kuweka usugu hivyo kutoangamizwa na kemikali hizo.
Wakati mwingine madawa ya kemikali yamesababisha madhara kwa watumiaji, mazingira na hata walaji hali iliyosababisha matumizi ya baadhi ya kemikali kupigwa marufuku na pia kuwekwa viwango vya kudhibiti ubora na usalama wa chakula.
Zifuatazo ni faida zinazothibitisha umuhimu wa njia za kiasili Gharama
Gharama ni kidogo ukilinganisha na madawa ya kemikali. Kwani vitu vinavyotumika kutengeneza madawa ya asili hupatikana kwa urahisi pasipo gharama kubwa na ambavyo huweza kupatikana au kuzalishwa shambani.
Usalama kwa binadamu
Matumizi ya kemikali yanaweza kudhuru afya ya mlaji. Madhara yanaweza kutokea kutokana na kutokufahamu maelezo ya matumizi. Aidha maelezo yanaweza kuandikwa kwa lugha isiyofahamika na mtumiaji.
Matokeo yake madawa haya yamesababisha harara ya ngozi, maumivu ya kichwa na hata saratani ya ngozi.
Kila mwaka, watu milioni moja huathirika kwa sumu itokanayo na matumizi ya kemikali. Kati ya idadi hii, watu 20,000 hufariki. Vifo hivi hutokea zaidi katika nchi zinazoendelea.
Usalama kwa mazingira
Dawa za kemikali katika kukabili wadudu na magonjwa huathiri mazingira kwa njia zifuatazo;
- Huua wadudu wenye manufaa.
- Dawa za kemikali zaweza kubakia kwenye mazingira na miili ya wanyama na kusababisha maafa siku za usoni.
- Wadudu na magonjwa huweza kuhimili dawa hizi baada ya kizazi fulani, hivyo basi kujenga usugu dhidi ya kemikali hizo.
Kutambua tatizo
Kabla ya kukabili magonjwa au wadudu ni vizuri kufahamu na kutambua tatizo lililopo. Unapofahamu na kutambua tatizo, unakua na uwezo wa kutibu aina ya madhara na vitu vinavyosababisha. Yanaweza kuwa ni ya hali ya hewa, upungufu wa madini au magonjwa yaliyosababishwa na wadudu. Kufahamu tatizo hupelekea kukabili au kuzuia kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Baadhi ya mbinu na njia za kiasili kukabili wadudu na Magonjwa
Udongo wenye rutuba
Udongo uliohifadhiwa kwa mfumo hai huimarisha viwango vya rutuba. Mimea yenye afya huweza kuhimili magonjwa na wadudu. Mimea inayolishwa vizuri katika udongo mzuri hujikinga zaidi na hatari za wadudu na magonjwa.
Madhumuni ya kutunza udongo ni;
- Kuboresha rutuba (viumbe hai) katika udongo
- Lishe kwa viumbe walio kwenye udongo
- Kupatia mimea madini yanayofaa ijapokua kemikali huimarisha afya ya mmea, matumizi yake yamekuwa na madhara kadhaa. Mmea waweza kuwa na kiasi kikubwa cha naitrojeni itokanayo na kemikali na kuufanya uvutie wadudu. Imebainika kwamba wadudu hutaga mayai katika sehemeu zenye mimea iliyo na naitrojeni nyingi ukilinganisha na mimea