Kilimo mseto ni njia ya kitamaduni, ambayo imekuwa ikitumiwa na wakulima barani Afrika na kwingineko tangu karne na karne.
Njia hii hutoa fursa kwa wakulima kuweza kuzalisha mazao mengi na ya aina tofauti katika sehemu ndogo ya ardhi. Hii ni kwa sababu mazao hayo hupandwa kwa pamoja katika eneo hilo.
Mbali na uzalishaji wa aina tofauti ya mazao, pia kilimo mseto hutoa fursa ya uzalishaji wa malisho kwa ajili ya mfugo, pamoja na uhifadhi wa mazingira.
Faidi nyingine ya kilimo mseto ni pamoja na udhibiti wa wadudu waharibifu pamoja na magonjwa kwa njia ya asili, kwa kuwa baadhi ya mimea inayopandwa pamoja hairuhusu uwepo na kuzaliana kwa wadudu wanaoweza kudhuru mazao hayo.