Ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha anauilisha udongo kwa kutumia virutubisho vya asili, ili kuweza kuwa na rutuba na kuzalisha mazao yenye tija.
Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu.
Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya
kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho.
Vipengele vingine vya ukuaji kama vile mwanga, nyuzi joto na maji viko katika hali inayofaa. Uwezo huu hautegemei kwenye wingi wa virutubisho kwenye udongo peke yake, lakini pia kwenye ufanisi wa kubadilisha virutubisho ndani ya duara la virutubisho shambani.
Sifa za udongo wenye rutuba
- Una virutubisho vingi muhimu kwa ajili ya lishe ya msingi ya mmea (ikiwemo naitrojeni,
fosfora, potashiamu, kalishamu, magnesia na salfa). - Una virutubisho vya kutosha vinavyohitajika kwa kiwango kidogo sana na mmea (ikiwemo boroni, kopa, chuma, zinki, manganizi, klorini na molibdenam).
- Una kiasi stahiki cha mabaki ya viumbe hai kwenye udongo.
- Una kipimo cha pH katika kiwango kinachofaa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao (kati ya 6.0 na 6.8).
- Una muundo unaomeng