Wakati jarida hili lilipozinduliwa mwaka wa 2011, moja ya mambo yaliyowakera wasinduzi na ambalo linaendelea kusumbua jamii ni mfumko wa bei ya vyakula. Jambo hili linawatatiza wakulima na walaji au watumiaji wa mazao ya kilimo. ˮ
Kuna sababu mseto zinazochangia kupanda na wakati mwingi kutotabirika kwa bei ya vyakula, na ambavyo lazima nchi kwa jumla ipambambane kudhibiti.
Nishati
Bei ya mafuta na gesi kuwa juu inasababisha uzalishaji, usagaji na usafirishaji wa nafaka kuwa juu sana, hivyo kufanya bei ya vyakula hivyo kuwa ghali pia.
Mtindo wa Ulaji
Katika nchi ambazo zinaendelea kwa haraka na uchumi wao kukua, tabia ya ulaji inabadilika. Uhitaji mkubwa wa nyama, inaongeza pia mahitaji ya nafaka kwa ajili ya mifugo. Hii inaleta ushindani mkubwa kati ya matumizi ya nafaka kuwalisha binadamu na mifugo.
Miji
Kutokana na kukua kwa majiji na miji ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo pia imekuwa ikipungua wakati idadi ya watu katika miji hiyo nayo ikiongezeka.
Nishati mbadala
Mataifa mengi yana kampeni ya uzalishaji wa nishati mbadala badala ya kutumia petrol kwa ajili yaviwanda, nishati ambayo inazalishwa kutokana na nafaka, hivyo nafaka nyingi zinatumika katika kutengeneza nishati mbadala kuliko chakula.
Hali ya hewa
Kimbunga, mafuriko na ukame ni baadhi ya mambo yanayosababisha mazao kuharibika au kufanya wakulima kushindwa kutumia ardhi yao kwa kilimo.
Utepetevu
Tatizo kubwa ni kwamba hatuko makini kuwa na mipango ya mbeleni. Tunafahamu kabisa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka, viwanda vinahitaji nishati, na tunafahamu kabisa kuwa wakulima wanahitaji pembejeo wanazomudu kununua.
Lazima tuwe makini katika kuweka sera na mikakati itakayosaidia kupambana na kutatua changamoto hizi zote. Tusiwe wepesi wa kulaumu!