Pale ambapo mbinu bora za kilimo zimetumika ipasavyo na bado kuna changamoto za wadudu na magonjwa, hakuna budi viuatilifu vya kilimo hai vikatumika au kwa kununua au kutayarishwa na wakulima wenyewe.
Viuatilifu ni moja ya pembejeo muhimu ya kilimo, kwani inasaidia katika ukizaji wa mazao haswa pale yanaposhambuliwa na magojwa pia wadudu wasumbufu. Mkulima unaweza kuzuia wadudu kwa kutumia mimea mbalimbali ya asili ambayo inapatikana katika mazingira yanayo kuzunguka. Katika hali ya kawaida sana, wakulima wanaposikia neno kiuatilifu hukimbilia kuwaza kemikali ya viwandani, la hasha1 katika kilimo hai tunazungumzia viuatilifu asili.
Katika picha hapa chini ni orodha ya mimea ambayo inaweza kutumika kama sehemu ya viuatilfu asili na wadudu ambao wanaweza kuzuiwa kwa mimea hio
Mkulima anaweza kutayarisha dawa ya kukabili wadudu kwa kutumia mchanganyiko wa mimea isiyopungua 18 na hii ni kwa ajili ya kukinga mimea aina zote kwa kufuata njia na taratibu zilizoainishwa hapo juu.
Matumizi ya dawa hizo
Tafadhali sana usizidishe vipimo isipokuwa kwa mazao ya muda mrefu kama mananasi, migomba, miti iIiyokwisha pandwa kwa muda mrefu shambani. Tafadhali usizidishe kwenye bustani ya maua nyumbani. Dawa hizi zina uwezo wa kuuwa wadudu waharibifu wa mmea na mazao ya aina yoyote na zina uwezo mkubwa pia wa kukinga na kutibu maradhi mengi yasababishwayo na wadudu. Pia zina uwezo wa kutibu, kukinga (ukungu) au kuvu ya majani kwenye mimea yako.
Aidha dawa hizi husaidia zaidi nguvu za ziada kwenye mmea wako iIi uweze kukua vizuri.
Mkulima akizingatia kanuni hizi ategemee kwamba atapata mazao mengi na bora, hivyo kuongeza kipato na kuinua hali ya uchumi katika maisha. Karibu viuatilifu vyote vilivyoainishwa hapo juu vinaweza kulimwa na mkulima mwenyewe.