- Kilimo

Dawa za asili kwa ajili ya kudhibiti wadudu kwenye mbogamboga

Sambaza chapisho hili

Kama ilivyo kwa aina nyingine ya kilimo kuwa na changamoto, wadudu pia ni moja ya changamoto inayowakabili wakulima wa kilimo hai na mara nyingi wamekuwa wakipambana kutafuta utatuzi.

Aidha, dawa mbalimbali za asili zimeonekana kufanya vizuri katika kudhibiti mashambulizi ya wadudu hawa kwenye mimea.

  1. Phytolacca Dodecandra

Mmea huu hutumika kama dawa ya kuulia wadudu kama vile aphids, mealy bugs, caterpillars, na wadudu wengine wenye ngozi laini.

Mchanganyiko wa dawa hii pia hutumika kwenye nyanya kuangamiza early late blight.

Tahadhari; Dawa hii isitumike wakati wa mavuno.

Namna ya kutengeneza

  • Chukua lita 10 ya maji kisha changanya na kilo 2 ya unga uliotokana na phytolaca
  • Chemsha kwa dakika chache mpaka utakapoona maji yamebadili rangi
  • Ongeza sabuni ya mche ukubwa wa kasha la kiberiti
  • Unaweza pia kuongeza vijiko 3 vya chai vya hamira ya chenga kabla ya kupulizia
  1. Marigold

Mmea huu hutumika kutengeneza dawa ya kudhibiti wadudu kama vile kimamba, mchwa, caterpillars, sisimizi na nematodes.

Namna ya kutengeneza

  • Chuma majani na maua ya marigold kiasi
  • Katakata au twanga kisha weka kwenye chombo
  • Ongeza lita 5 za maji kisha funika
  • Acha kwa muda wa siku 5 hadi 10 huku ukikoroga kila siku.
  • Baada ya siku 10 itakuwa imeoza
  • Chuja kuondoa maji maji yale kisha masalia yanawza kutumika shambani kama matandazo kwenye bustani ya mbogamboga
  • Chukua maji yale kisha changanya na sabuni kwa uwiano wa 1 kwa 1 kwa sabuni ya unga, 1 kwa 16 [vipande 16 vyenye ukubwa wa kasha la kiberiti] kwa sabuni ya mche, na 1 kwa 2 [chupa mbili za soda au bia] kwa sabuni ya unga
  • Nyunyizia kwenye eneo la mmea lililoathiriwa na wadudu
  1. Tephrosia

Mmea wa tephrosia hutumika kutengeneza dawa ya kudhibiti wadudu kama vile aphids, mealy bugs, mchwa na sisimizi.

Namna ya kutengeneza

  • Chuma majani 5 ya mmea huu kisha weka kwenye maji
  • Loweka kwa muda was aa 24 yaani siku moja
  • Chuja na nyunyizia kwenye mimea
  1. Black jack

Mmea huu hutengeneza dawa ya kudhibiti wadudu kama vile aphids, mealy bug, ants, beetles, bollworms, termites and mites.

Namna ya kutengeneza

  • Kusanya mbegu kiasi cha gramu 500 za black jack
  • Chemsha kwenye maji lita 2 kwa dakika 10
  • Epua na acha ipoe kisha ongeza maji lita 3 na sabuni kijiko kimoja cha chai kisha puliza mara baada ya kuchanganya.
  1. Neem leaf

Dawa inayotokana na mmea huu hutumika kudhibiti wadudu kama vile aphids, mealy bug, beetles, caterpillars.

Namna ya kutengeneza

  • Kusanya kilo 1 ya majani ya neem kisha twanga
  • Changanya na lita 10 za maji kisha koroga kwa muda wa dakika 10
  • Chuja vizuri kupata juisi kisha ongeza sabuni ukubwa wa kasha la kiberiti na nyunyizia kwenye mimea yaliyoathirika.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *