- Shuhuda

Miaka 10 ya Mkulima Mbunifu na kilimo hai

Sambaza chapisho hili

Mkulima Mbunifu imechangia kwa asilimia kubwa kufahamika na kutekelezwa kwa kilimo hai nchini Tanzania. Hii ilikuwa ni ndoto ambayo imegeuka na kuwa kweli.

Watanzania wengi na baadhi ya wakulima wa nchi jirani wameelimika na kufahamu kwa kina kuhusu kilimo endelevu kupitia MkM. Ninafuraha kubwa kushiriki katika kuifanya ndoto hii kutimia na kuendelea kuwa msaada kwa uwepo wake.

Wazo la uwepo wa MkM lilianza mwaka 2010, na kutekelezwa kuanzia June 2011, ambapo kufikia mwezi Agosti Jarida la kwanza la MkM lilizinduliwa katika maonesho ya wakulima yaliyokuwa maarufu Nane Nane katika viwanja vya Themi Njiro jijini Arusha.

Mwanzo huo ulikuwa ni kama taa katika giza nene kwani lilikuwa ni jarida pekee na la kwanza kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo, ufugaji, na mazingira. Halikadhalika kutoa njia ya uwepo wa taarifa nyinginezo za kilimo. Mradi ulizinduliwa kukiwa na uwezekano wa kuchapa nakala 500 tu na kuzitoa kwa vikundi vya wakulima hapa nchini.

Upekee wa MkM si kwa utoaji wa taarifa za kilimo tu ila aina ya taarifa hizo na umuhimu wake, kwani limeangaza kwa kina njia sahihi za kilimo hai, Wanyama na mifugo. Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa mradi huu umeweza kukua na kuchapisha nakala 15,000 kwa mwezi ambazo bado hazitoshi, halikadhalika kuwafikia wakulima kwa njia ya mtandao, na vipindi vya redio.

Ni furaha kubwa kuona watu wengi wakiwemo vijana wamehamasika katika njia sahihi za kufua kilimo kwa kurutubisha udongo kwa njia za asili ambazo zimefundishwa kupitia MkM. Ufugaji wa asili wenye tija umeshika hatamu. Tafiti zinazolenga utunzaji wa mazingira, uzalishaji endelevu zimeweza kuvumbuliwa na kuwekwa wazi kwa wakulima kwa njia rahisi ambayo wameweza kuzitumia.

Ninapongeza timu ya MkM na washirika wake ambao wameendelea kusukuma mbele gurudumu hili muhimu katika nyanja ya kilimo hai na namna juhudi mbadala zinavyofanyika kila uchao kuhakikisha kuwa wakulima na jamii nzima ya jumuia ya Afrika ya Mashariki hawarudi nyumba kugeukia tena matumizi ya kemikali, jambo ambalo limeimarisha afya kama ilivyokusudiwa.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 maoni juu ya “Miaka 10 ya Mkulima Mbunifu na kilimo hai

    1. Habari
      Karibu sana Mkulima Mbunif na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za Mkulima Mbunifu.

      Tafadhali nakutumia kiambatanishi kwenye barua pepe yako. Asante

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *