- Kilimo

Fahamu udongo wako ili kuboresha usimamizi wa rutuba

Sambaza chapisho hili

 

Kuna virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ukuaji wa mmea. Upungufu wa mojawapo ya virutubishi hivi muhimu utapunguza ukuaji wa mimea. Mavuno yanategemea kiwango cha virutubisho muhimu kwa mmea.

Mimea yote hutegemea vitu muhimu kukua vizuri. Vitu hivi vinaweza kugawanywa mara mbili;

  • Vitu vya madini, kupitia udongo.
  • Vitu visivyo vya madini: haidrojeni, oksijeni, na kaboni ambazo zinapatikana kwa wingi katika anga na kwenye mvua au maji.

Madini muhimu

Udongo wenye rutuba una virutubisho vyote vikuu kwa lishe ya msingi ya mimea. Virutubisho hivi ni pamoja na nitrojeni, fosforasi, potasiamu, kalsiamu, magnesiamu na salfa, ambazo zikikosekana hudumaza ukuaji wa mimea.

Virutubisho vingine vinavyohitajika ni pamoja na chuma, zinki, shaba/kopa, boroni, molibdenamu, Manganisi, klorini, na nikeli.

Kawaida mchanga wenye rutuba pia utakuwa na mabaki ya viumbe hai ambavyo vinaboresha muundo wa mchanga na kuleta uhai wa kibiolojia, uhifadhi wa unyevu wa udongo, na pia utunzaji wa virutubisho.

pH – Viwango vya asidi (tindikali) inadhibiti upatikanaji wa virutubishi, ukuaji wa mimea na afya ya vijidudu kwenye udongo. Mimea hukua vizuri ikiwa udongo una vipimo vya asidi kati ya 6 na 7.

Haya yote kwa pamoja yanakupatia udongo unaoweza kuzalisha mimea yenye afya na kupata mavuno ya juu.

Changamoto

Kwa bahati mbaya, udongo katika maeneo mengi hauna viwango vya kutosha vya virutubisho vyote vinavyohitajika kwa ukuaji wa mimea.

Changamoto kubwa za kudumisha rutuba sahihi ya mchanga, ni;

  • Matumizi duni ya mbolea zinazofaa na mbinu dhaifu za marekebisho kwa kutumia mbinu hai, kwa mfano, samadi au masalio ya mimea.
  • Viwango vya juu vya tindikali (asidi) kutokana na kutumia mbolea mingi ya viwandani (hasa, Diammonium Phosphate – DAP), matumizi mbaya ya mbolea, kumwagilia shamba maji yenye chumvi, na mbinu zisizofaa zinazosababisha mmomonyoko wa udongo.
  • Ukosefu wa uwezo wa kutambua vizuri hali ya rutuba ya udongo, ambayo inaweza kubainisha vizuizi vikuu kwa uzalishaji wa mazao.

Mbinu za kurekebisha udongo

  • Hatua ya kwanza katika kurekebisha na kuboresha rutuba ya udongo ni kujua hali ya udongo. Hii itawezekana kupitia kupima na kuchambua udongo kwenye mahabara ili kujua upungufu wake na marekebisho yanayofaa. Tembelea Afiwa wa Kilimo katika eneo lako kujua huduma za kupima udongo zinazopatikana karibu na wewe, ziwe za serikali ama za kibinafsi.
  • Ikiwa udongo una asidi ya juu (ya pH chini ya 6) basi rekebisha kwa kutumia chokaa (lime). Chokaa inapunguza asidi na kuongeza madini ya kalsiamu na magnesiamu. Chokaa pia hufanya fosforasi ambayo imeongezwa kwenye mchanga kupatikana kwa ukuaji wa mimea, na huongeza upatikanaji wa nitrojeni kwa kuharakisha kuoza kwa vitu vilivyo hai kama masalio ya mimea na kinyesi cha mifugo. Chokaa inapatikana kwa wakala wa pembejeo.
  • Ikiwa mkulima hana hela za kununua chokaa madukani, anaweza kutumia jivu kutoka jikoni. Hii inaweza kuchanganywa na kinyesi cha mifugo au wakati wa kutengeneza mbolea mboji.
  • Tumia mbinu za kurekebisha tabia ya udongo kwa kuogeza kaboni. Mbinu hizi ni kama mabaki ya mazao na majani ya miti, kinyesi cha mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kuku, kondoo, na kadhalika, na pia mboji. Hii pia, inasaidia mizizi ya mimea kuingia kwa udongo kwa urahisi na kunyonya virutubisho.

Kumbuka rutuba ya udongo unajumuisha mwingiliano wa vitu tatu; madini, muundo wa udongo na uwepo wa virubishi vya kibiolojia au viumbe hai. Kufuatana na hili, ukuaji na nguvu ya mimea, nguvu na mavuno hutegemea upatikanaji wa virutubishi muhimu.

Ikiwa mkulima atazingatia afya ya udongo wake na kuhakikisha analisha udongo, basi udongo pia utalisha mimea na kuleta mavuno mengi nay a hali ya juu.

Madini 14 muhimu kwa ukuaji wa mimea (Make a box)

Nitrogeni – inahitajika kwa shughuli ya kutengeneza chakula cha mmea na rangi ya kijani kibichi (chlorophyll) ili kunyonya nguvu kutoka miale ya jua. Ukosefu wa nitrojeni husababisha upotezaji wa nguvu na rangi. Ukuaji unakuwa polepole na majani huanguka, kuanzia chini ya mmea. 

Fosforasi – huchochea ukuaji wa mizizi na maua. Inahusika katika kusafirisha na kuhifadhi nguvu au virutubisho vya nguvu kwa mmea. Inaboresha hali ya jumla ya mmea na huongeza uwezo wa mmea kuhimili hali mbaya ya hali ya hewa. Uhaba wa fosforasi utoaji wa maua, maua huwa chache na hafifu. Pia, matawi ya mmea huwa ya rangi kahawia na iliyokunjana, na mmea huwa hafifu.

Potasiamu – hutumika kudhibiti maji na usafirishaji wa vitu vya akiba ya mmea. Inaongeza uwezo wa mmea kutengeneza chakula (usanisinuru), inaimarisha tishu za seli, na inamsha unyonyaji wa nitrogen. Pia, huchochea utengenezaji wa maua, virutubishi vya nguvu. Inawezesha mmea kuhimili mazingira yasiyofaa kama baridi kali na joto la juu (kunyauka).

Ukosefu wake upunguza uwezo wa mmea kuhimili baridi, joto, mashambulizi ya kuvu na vimelea wengine. Hii usababisha ukosefu wa usawa kati ya madini mengine, hasa kalsiamu, magnesiamu, na nitrojeni. Ukosefu wa Potasiamu unajionyesha kupitia madoadoa meusi kwenye majani.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *