Wafugaji wamekua wakijisahau juu ya umuhimu wa chanjo kwa mifugo, Katika msimu wa mvua za masika, mifugo mingi imekua ikiathirika kutokana na magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bacteria pia virus.
Wafugaji wa kuku haswa wakienyeji, wameishia kupoteza mifugo yao kutokana na kutozingatia chanjo. Mara nyingi mvua hizi huambatana na magonjwa mengi kwa kuku kama vile gumboro, ndui ya kuku, kideri, kipindupindu na mengineyo.
Kutokana na kuku kushambuliwa sana na magonjwa haya ambayo hupelekea maambukizi ya haraka na vifo, ni muhimu kwa wafugaji kuhakikisha wanawapatia kuku chanjo kwani magonjwa mengi hayana tiba.
Wasiliana na maafisa ugani katika eneo lako kwa ushauri zaidi kuhusu muda sahihi na aina ya chanjo mahususi kwa kuku unaofuga. Mkulima Mbunifu ipo kukushauri juu ya chanjo na udhibiti wa magonjwa yanayo ambatana na msimu wa masika.