Ili uweze kufanya kilimo hai ni lazima uwe na mbolea za asili. Bila mbolea za asili huwezi kufanya kilimo cha aina yeyote kwa misingi ya kilimo hai.
Mbolea za asili zipo za aina mbalimbali ama huweza kutengenezwa kwa njia mbalimbali na kwa kutumia malighafi mbalimbali kama vile samadi, majani ya kurundika nakadhalika.
Baadhi ya mbolea za asili na njia za kuzalisha mbolea za asili ambazo mkulima wa kilimo hai huweza kutumia katika kilimo kwa ajili ya uzalishaji bora ni pamoja na mabaki ya mazao, mazao funikizi, matandazo, samadi ya ng’ombe na mboji.
Mbolea za asili zina faida kuu mbili, moja huongeza na kushamirisha viumbe hai katika udongo na pia ni huru kwani unaweza kuotesha au kutengeneza mwenyewe. Na pia kama utakuwa na mbolea nyingi kupita mahitaji yako, unaweza kuuza na ikanunuliwa.
Hata hivyo baadhi ya mbolea za asili zinakosa kirutubisho muhimu cha kutosha cha fosiforasi ambayo mmea huhitaji kwa ajili ya kukua. Hata hivyo, unaweza kuongeza ubora wa mbolea za asili kwa kuongeza mimea yenye virutubishi vya fosifirasi kwa wingi.
Mabaki ya mimea
Mabua na majani ya baadhi ya mazao ni mazuri sana kwa matandazo. Stover kutoka kwenye mahindi na mtama huanza kuoza taratibu nhivyo hukaa juu ya ardhi kwa muda mrefu kido na kufanya kufunika udongo.
Aidha, mabua na majani ya mikundeyana wingi wa naitrojeni na huoza kwa haraka hivyo kuwezesha virutubishi kutumika kwa haraka kwa mimea itakayofuata kuoteshwa.
Kinyesi cha wanyama (samadi)
Samadi inayotokana na kinyesi cha wanyama ni mbolea nzuri sana katika kilimo hai. Aidha, baada ya kukusanya kinyesi hiki kutoka kwa wanyama, iachwe ili iweze kuoza kabla ya kupeleka shambani kwani ukiweka moja kwa moja ikiwa imetoka kwa wanyama ikigusa mimea huweza kuunguza.
Kinyesi kinachotokana na kuku hutengeneza pia mbolea nzuri sana kwa ajili ya kilimo hai ikifuatiwa na kinyesi cha mbuzi, kondoo na kinyesi cha ng’ombe.