1.0 MUHTASARI WA MWENENDO WA MVUA KWA TAREHE 11-20 MACHI, 2026 NA MATARAJIO YA MVUA KWA TAREHE 21-31 MACHI, 2026.
1.1 MUHTASARI WA MWENENDO WA VIASHIRIA NA MIFUMO YA MVUA TAREHE 11-20 MACHI, 2026.
Katika kipindi hiki, migandamizo mikubwa ya hewa iliyopo kusini mwa dunia (St. Helena na Mascarene) iliendelea kuimarika kidogo wakati ile iliyopo kaskazini mwa dunia (Azore na Siberia) iliendelea kudhoofika kidogo. Hali hii ilisababisha ukanda mvua kuendelea kuwepo katika baadhi ya maeneo ya Ukanda wa ziwa Victoria, magharibi mwa nchi, kanda ya kati, kusini na nyanda za juu kusini magharibi. Kwa upande mwingine joto la bahari katika eneo la magharibi mwa bahari ya Hindi lilikuwa la wastani hadi chini ya wastani. Hali hii ilipelekea kuimarisha mifumo isababishayo mvua katika maeneo ya ukanda wa pwani na nyanda za juu kaskazini mashariki.
Kwa maelezo zaidi soma hapa https://www.meteo.go.tz/uploads/text-editor/files/Dekad%2021%20-%2031%20March%20%202026%20Kiswahili_1774019175.pdf


