- Kilimo, Kilimo Biashara

Ukizingatia kanuni hizi utafanikiwa kuwa na uzalishaji bora wa mazao

Sambaza chapisho hili

 

  1. Usafishaji wa shamba. Shamba likiwa safi unapunguza sehemu ambazo wadudu wanaweza kuzaliana kwa urahisi, pamoja na sehemu ambazo vitu vinavyosababisha magonjwa vinaweza kujificha. Mkulima anashauriwa kupalilia shamba lake mara kwa mara na kila inapowezekana kuhakikisha anaondoa masalia ya mazao ya msimu uliopita shambani. Masalia hayo yakibaki shambani wadudu wa magonjwa ya mazao hayo vitaendelea kuwepo na kuzidi kuzaliana.
  2. Kilimo cha mzunguko Unapolima zao la aina moja kwenye eno moja kwa muda mrefu, magonjwa na wadudu wa zao hilo vitaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Mkulima anapaswa abadilishe mazao kila msimu. Mazao yatakayopandwa kwenye mzunguko yawe ya jamii tofauti. Hii ina maana kuwa yawe yanashambuliwa na wadudu na magonjwa tofauti na msimu uliopita.
  3. Upandaji wa mbegu vumilivu Kila inapowezekana tumia aina yambegu inayostahimili uharibifu wa magonjwa na wadudu (resistance varieties) ambazo hazishambuliwi kwa urahisi.
  4. Matumizi ya mbolea ya samadi/ mboji Mkulima anapotumia mbolea ya kutosha kwenye mazao yake mimea inakuwa na nguvu hivyo inastahimili mashambulizi ukilinganisha na mimea ambayo haina mbolea kabisa.
  5. Matumizi ya mbegu bora na safi Wakati wa kuchagua mbegu, mkulima anapaswa kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea iliyo bora katika shamba lake. Ukichukua mbegu kutoka kwenye mmea wenye ugonjwa utahamisha ugonjwa huo kutoka eneo moja hadi lingine na hata kutoka msimu mmoja hadi mwingine. Hakikisha kila inapowezekana mbegu zinanunuliwa kutoka kwenye maduka yanayoaminika. Endapo utalazimika        kutayarisha  mbegu, hakikisha unazipata kutoka kwenye miche iliyo bora, na yenye afya nzuri. Tofauti na hapo hakikisha unanunua mbegu kutoka kwenye makampuni ya mbegu yaliyosajiliwa.
  6. Kupogoa Kila mkulima anapoona dalili za ugonjwa, ni muhimu kuondoa sehemu yenye ugonjwa kwenye mmea. Kwa mfano, ugonjwa wa ukungu kwenye nyanya. Unapoona dalili za kwanza za ugonjwa huo kwenye jani, basi tahadhari ya kwanza ni kuiondoa sehemu ya majani yenye ugonjwa ili usienee kwenye majani au mimea mingine.
  7. Kutandaza nyasi (Mulching) Mbali na kuzuia magugu yasiote kwa urahisi, pia matandazo huzuia baadhi ya magonjwa yasishambulie mazao. Kwa mfano, ugonjwa ambao viini vyake vinaweza kujificha ardhini, unapotandaza nyasi viini vya ugonjwa visisambae kwa urahisi hasa kama ugonjwa huo unaenezwa kwa njia ya matone ya mvua au upepo mfano magonjwa ya ukungu (blights) uozo mweusi (Black rots) na mengineyo.
  8. Uzuiaji wa magonjwa na wadudu Kinga ni bora kuliko tiba, inashauriwa kuzuia visumbufu kabla ya kuleta mad hara.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *