- Kilimo, Kilimo Biashara

Siku ya chakula duniani October 2024

Sambaza chapisho hili

Siku ya chakula duniani ni maadhimisho ambayo yaliwaleta pamoja wadau wa kilimo na chakula kutoka sehemu mbalimbali. Hata hivyo siku hii ilikuja huku kukiwa na mvutano na mizozo ya kimataifa na majanga ya tabianchi ambayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia changamoto ya mamia ya mamilioni ya watu duniani kote kukabiliwa na njaa na mabilioni ya watu kushindwa kumudu chakula bora.

Katika kuhakikisha lishe inakuwa jambo la msingi kwa wote katika maadhimisho ya siku ya chakula dunianai mradi uliweza fanya maadhimisho haya kupitia chakula cha asili ambacho kilizingatia usalama wa vyakula na namna mbalimbali za uandaji wake kwa kujali ulindaji wa virutubishi.

Lishe husaidia ukuaji sahihi, na tunashauri matumizi ya bidhaa mbalimbali za asili ambazo ni safi na salama.

Matumizi mbali mbali ya vyakula ilikulinda afya na kuwa na lishe bora

Vyakula vingi vya asili vilivyotumika miaka ya nyuma vimekuwa na ubora wa kilishe na kulinda miili yetu na kutukinga na magonjwa mbali mbali. Hivi vyakula vimekuwa vikichanganywa na vitu mbalimbali;

  • loshoro mchanganyiko wa mahindi na maziwa mgando (wanga na protini) na wengine huongeza aina ya ndizi maarufu Mkoani Arusha kwa jina la ndizi ng’ombe.
  • Ngitalolo mahindi, maharagae, maziwa na mboga za majani (wanga, protini na vitamini)
  • Matoke ndizi, maharage, nyama (wanga, protini ya kutosha)
  • Sharubati mbalimbali kama vile rosela, ubuyu, ukwaju
  • Matumizi ya bidhaa kama kweme inayoaminika kama kiungo cha mboga (protini)

Elimu ya uandaaji sahihi wa vyakula vya asili ni muhimu sana kwa mfano:

  • Epuka kutengeneza loshoro itakayokaa muda mrefu sana kwenye kibuyu na kuendelea ongeza maziwa.
  • Epuka kuloweka mahindi kwa muda mrefu na kutwanga kwa matumizi hii hupoteza nguvu na ubora wa wanga.
  • Kuosha mahindi au maharage kwa kutumia magadi , hakikisha utayapika kwa kuongeza viungo au kutumia mboga za majani pembeni ili kurudisha virutubisho ulivyopoteza.

Ikumbukwe kuna baadhi ya vyakula hutumiwa sana nchini Tanzania kama vile ugali (sembe/dona), makande, chapati, mboga za majani

Vyakula hivi vinaweza ongezewa thamani zaidi kwa kuongeza ubora

  1. Ugali; tuache dhana ya kutumai ugali wa mahindi peke yake unaweza changanya mahindi na mbaazi/ njugu mawe/ boga. Hapa tunapata ongezeko la protini kwenye ugali wetu hata vitamini zingine kama B
  2. Makande; tumezoea kuchanganya mahindi na maharage tu ila unaweza weka mahindi, maharage, mbaazi, njugu mawe, ngano na karanga pia na viungo kama karoti, kitungu na nyanya. Hapa tunakuwa na mlo kamili
  3. Chapati; tumekuwa na tabia ya kupika kutumia ngano peke yake bali unaweza changanya na boga au kiazi lishe hii inasaidia kupata vitamini A zaidi
  4. Mboga za majani; kwa mazoea zaidi huwa viungo kama karoti na kitungu huwekwa kwa kiasi kidogo ila tunaweza ongeza kiwango cha hivi viungo ilikuwa na mboga zenye kiwango kikubwa cha virutubisho.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Afisa lishe kutoka shirika la Iles De Paix (IDP) Monica Michael Morrison.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *