- Mifugo

Ufugaji bora wa ng’ombe unaoleta tija kwa mfugaji

Sambaza chapisho hili

Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi, mbolea na hutumika kama wanyama kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa.

Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa. Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na Ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na;

  • Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji huria.
  • Kujenga banda au zizi bora.
  • Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
  • Kutunza makundi mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
  • Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na
  • mahitaji ya mwili.
  • Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.
  • Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana
  • na mahitaji ya soko.
  • Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango
  • vya ubora na usalama.
  • Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu
  • ya ufugaji.

Mifumo ya ufugaji

Ng’ombe wanaweza kufugwa katika mfumo wa ufugaji huria au kulishwa katika banda (ufugaji shadidi). Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho mazurim na vyanzo vya maji.

Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho. Ufugaji wa shadidi uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi.

Ufugaji wa mfumo huria

Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-

  • Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao.
  • Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikana wakati
  • Awe na eneo lenye maji ya kutosha na
  • Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe
  • \kuzaa bila mpangilio.

Matunzo mengine ya ng’ombe yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri hatua ya uzalishaji na matumizi ya ng’ombe husika. 

Banda/zizi bora la ng’ombe

Banda bora

Banda lijengwe sehemu ya mwinuko mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-

  • Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na baridi.
  • Kuta imara zenye matundu au madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na mwanga wa kutosha,
  • Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na uchafu kutuama.
  • Lijengwe katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi kila siku, na sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuweka malalo.
  • Paa lisilovuja.

Aidha kwa wafugaji wanaofuga katika ufugaji huria ambako mazizi hutumika, inashauriwa kuzingatia yafuatayo;

  • Zizi likae mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama
  • Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya wezi na Wanyama hatari.
  • Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo ng’ombe watengwe kulingana na umri wao.
  • Zizi lifanyiwe usafi mara kwa mara
  • Liwe na sehemu ya kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya vyakula, sehemu ya kutolea huduma za kinga na tiba, eneo la kulishia na maji ya kunywa.

Zizi bora

Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko isiyoruhusu maji kutuama mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo;

  • Liweze kuhakikisha usalama wa ng’ombe.
  • Ukubwa wa zizi uzingatie idadi ya mifugo.
  • Liwe na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa usafi mara kwa mara.
  • Zizi la ndama liwe na paa imara.
  • Lijengwe kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi.

Uchaguzi wa koo na aina ya ng’ombe wa kufuga

Kwa ufugaji wenye tija, mfugaji anashauriwa kuchagua koo na aina ya ng’ombe kwa kuzingatia malengo ya ufugaji (nyama au maziwa).

Ng’ombe wa nyama

Ng’ombe wanaofaa kufugwa kwa ajili ya uzalishaji nyama ni wale wanaokua kwa haraka na kuweka misuli mikubwa iliyojengeka vizuri. Baadhi ya koo zenye sifa hizo ni Pamoja na Boran, Mpwapwa (nyama na maziwa), Charolais, Aberdeen Angus, pamoja na chotara wao. Hata hivyo, nchini Tanzania ng’ombe aina ya Zebu (mfano Ufipa, Gofo, Masai, Sukuma, Tarime, Iringa red), Sanga (Ankole) na chotara wao ndio hutumika kama ng’ombe.

Ng’ombe wa maziwa

Sifa za ng’ombe wa maziwa zifuatazo;

  • Umbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani.
  • Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani.
  • Miguu ya nyuma mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara.
  • Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu na unene wa wastani
  • Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha na
  • Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa.

Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, Jersey, Mpwapwa, Simmental na chotara watokanao na mchanganyiko wa aina hizo na Zebu.

Utunzaji wa makundi mabalimbali ya ng’ombe wa maziwa kulingana na umri na hatua ya uzalishaji

Utunzaji wa ndama

Mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya maziwa.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na

  • Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tinture of Iodine) mara baada ya kuzaliwa na
  • Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara baada ya kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Aidha, aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.

Endapo jike aliyezaa amekufa au hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo;

  • Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
  • Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
  • Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oili).
  • Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3 na yai moja bichi. Koroga mchanganyiko huo, weka katika chupa safi na ndama anyweshwe kabla haujaopoa. Ndama anyweshwe mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *