- Kilimo

Kitunguu saumu kama dawa ya asili

Sambaza chapisho hili

Kitunguu saumu pia kinaweza kuwa mbadala wa kudhibiti viwavi, nzi wa matunda, utitiri mwekundu, utitiri mweupe, wadudu wenye magamba laini, kombamwiko wa madoa, magonjwa ya fangasi na minyoo fundo.

  • Menya kilo mbili za kitunguu saumu na uzitwange vizuri (tumia blenda ni vizuri zaidi).
  • Ongeza mililita 500 za maji ili kusaidia kukamua juisi/ mchanganyiko.
  • Tumia chujio kupata mchanganyiko wa kitunguu saumu.
  • Weka kwenye chupa au chombo maalumu na ongeza maji kutengeneza lita 10 za mchanganyiko.
  • Weka mchanganyiko huo kwenye chombo kilichofunikwa. Weka alama kwenye chombo hicho.
  • Kwenye mchanganyiko wa lita 10, toa lita moja na weka kwenye bomba la kunyunyiza, ongeza lita 15 za maji ili kukamilisha tanki zima, na ongeza mililita 10 za sabuni kimiminika.

Nyunyiza wakati wa asubuhi au jioni kwenye mimea iliyoathiriwa. Nyunyiza kila baada ya wiki moja.

Mchanganyiko huo unaweza kutumika ndani ya miezi 3.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *