Parachichi ni moja ya zao la matunda ambalo liko katika kundi la mmea wenye ghala mbili, yaani tunda lake hulizunguka peke linalokuwa ndani, kitalaamu parachichi huitwa Persea Americana, parachichi lipo katika kundi la maua kupandwa, umbile la parachichi ni mviringo au yai. Mti wa parachichi unajichevusha wenyewe. Parachichi kibiashara linafaida maana linahitajika sana kiafya.
Faida za Parachichi upande wa Lishe
Tunda la parachichi lina vitamini zifuatazo;
- Lina Vitamini A: Husaidia kuimarisha macho na kuipa uwezo wa kuona vizuri.
- Lina Vitamini B (B1-B12): Husaidia mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasawa na kuuepusha mwili na matatizo ya misuli.
- Lina Vitamini C: Husaidia kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa.
- Lina vitamini D: Husaidia kuimarisha mifupa ya mwili.
- Lina vitamini E: Husaidia kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi.
- Lina vitamini K: Husaidia kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu.
Madini- (Mineral Elements)
Ni tunda lenye
- Madini ya Chuma kwa wingi (Fe): Haya husaidia katika utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oksijeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi.
- Madini ya kalsiamu: Lina madini ya kalsiamu, yanayosaidia kwenye ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili.
- Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa mwilini
Maoni kupitia Facebook