Fahamu faida ya mpera, tunda na majani yake kiafya
Matunda ya asili yana utajiri wa sukari, madini, vitamini na viini muhimu kwa ajili ya tiba ya magonjwa ya binadamu na mifugo. Matunda yanaweza kuwa chanzo muhimu sana cha chakula, lishe na madawa. Hivyo yanaweza kusaidia kupiga vita utapiamlo na upungufu wa vitamin A na C, amino asidi muhimu na madini kama chuma na zinki.
Katika Makala hii tutaangazia mmea wa mpera na faida zake.
Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamin A na C, madini ya potassium, nyuzinyuzi za fiber, vyote hivi ni muhimu kwa afya ya mwanadamu. Mapera ni matunda yanayopatikana kwa wingi lakini mara nyingi huwa hayapendwi sana kutokana na ugumu wake wakati wa kuyatafuna pamoja na kuwa na mbegu mbegu nyingi. Hata hivyo matunda haya yana faida kubwa sana kwa afya ya mwili wa mwanadamu. Pera linaweza kutumika kama tunda ama kutengeneza juisi
Zifuatazo ni faida za mapera
- Utajiri wa Vitamin C ambayo ni muhimu katika mwili wa mwanadamu.
- Ni kinga nzuri ya kisukari. Ulaji wa watu wengi unawaweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari lakini matumizi ya mapera yatakupunguzia hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari, hii ni kwa sababu mapera yana utajiri mkubwa sana wa nyuzinyuzi. Nyuzinyuzi ni muhimu sana katika kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu. Vilevile ni muhimu sana katika kuusafisha mfumo wa usagaji wa chakula
- Kuimarisha uwezo wa kuona. Mapera yana utajiri mkubwa sana wa Vitamin A au Retinol ambayo ni muhimu sana katika kusaidia kuona vizuri. Hivyo basi kama ilivyo kwa karoti, mapera yanasaidia sana katika kuongeza na kuimarisha uwezo w a mtu kuona.
- Kusaidia katika Uzazi. Mapera yana madini yaitwayo Folate ambayo husaidia katika kurutubisha mayai ya uzazi.
- Kurekebisha kiwango cha shinikizo la damu. Madini ya Potassium yaliyomo ndani ya mapera yanasaidia katika kukurekebisha shinikizo la damu (Blood Pressure).
- Utajiri mkubwa wa madini ya shaba. Mapera yana madini ya shaba (Trace element copper) ambayo ni mazuri sana katika kumaintain ufanyaji kazi wa tezi ziitwazo thyroid. Tezi za thyroid zisipo fanya kazi vizuri zinaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya kwa mwanadamu.
- Utajiri wa madini ya manganese. Mapera yana utajiri mkubwa wa madini ya manganese ambayo yanausaidia mwili katika kunyonya ama kupata virutubisho muhimu kutoka kwenye vyakula tunavyo kula. Chakula tunacho tumia kikitumika vizuri mwilini, tunapata virutubisho vyote muhimu kama vile biotini, vitamin nakadhalika.
- Kuusadia mwili na akili katika kupumzika. Mapeara yana utajiri mkubwa wa madini ya magneziamu ambayo hufanya kazi ya kuvifanya akili na mwili wa mwanadamu viweze kupumzika. Unashauriwa kutumia mapera baada ya kazi nzito. Hii itasaidia katika kuufanya mwili na akili yako kupumzika
- Mapera ni muhimu katika afya ya akili ya mwanadamu. Vitamin B3, Vitamin B6 ambazo zinapatikana ndani ya tunda la mpera muhimu katika kuimarisha afya ya akili ya mwanadamu. Mapera yatasaidia kuufanya ubongo kupumzika.
Faida ya majani ya mapera
- Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na kikohozi.
- Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy).
- Pia majani haya ya mpera yakichemshwa kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi mwilini.
- Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini.
- Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.
- Pia inatumika kama scrub ya uso. Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni.
- Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa ya kuponyesha tumbo la kuhara.
- Kama umejikata kidogo unaweza kutumia majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri kwa kupunguza maumivu na kukulinda na maambukizi ya bakteria.
- Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu eneo la mwili lililong’atwa na mdudu na kupunguza maumivu.
- Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina uwezo wa kutibu tezi dume.
- Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi majani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibu chunusi.
- Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguza uzito mwilini na kuzuia uharibifu sukari ndani ya mwilini.
- Majani ya mpera yanajaza nywele na kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya nywele zako.
- Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi, maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mpera na utaona maajabu ya majani haya.
- Chukua majani ya mpera saga vizuri mpaka yawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kisha tumia kupaka usoni kama scrub inatibu ngozi inayoanza kuzeeka mapema.
- Chai ya mpera inasaidia kwa kutibu mvurugiko wa tumbo.
- Majani ya mpera yanaondoa tatizo la kukatika kwa nywele. Chemsha majani kisha wacha yapoe na ukande kwenye paji na eneo la ngozi taratibu kwa dakika 15, Wacha kwa dakika 30 kisha osha na maji safi bila shampoo au sabuni. Fanya hivyo mara 3 kila wiki.
Muhimu: Kuna namna mbili. Aidha chemsha maji kama glasi nne mpaka yachemke sana, chukua majani kama 10 ya mpera, weka ndani ya maji ya moto alafu funika kwa dakika 10 – 15 koroga chuja, chai yako Tayari.
Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani yakiwa ndani. Ikikokota ondoa kwa moto, wacha kwa dakika 10 -15 chuja, chai tayari. Waweza kutumia majani yaliyokauka pia. Kabla sijasahau ni vizuri zaidi ukichanganya na asali badala ya sukari.
Swali? Je wewe unasoma jarida ukiwa mkoa gani? Tutajie matunda ya asili yanayotumiwa zaid katika mkoa wako?