- Kilimo

Upotevu unaotokea katika mfumo wa shughuli za baada ya kuvuna

Sambaza chapisho hili

Upotevu wa chakula ni upungufu wa kiasi na ubora wa chakula. Hii inatokana na ukweli kwamba mazao yaliyovunwa yana uhai; hupumua na hupitia mabadiliko wakati wa shughuli za baada ya kuvuna. Kwa mazao makavu kama vile nafaka na kunde yasiyoharibika kwa urahisi, upotevu hujitokeza kama matokeo ya uharibifu usababishwao na viumbe waharibifu au vitu vingine, ambao huchukua sehemu ya chakula inayopatikana au kusababisha uharibifu, kuzorota na kuharibu kiwango ambacho bidhaa iliyobaki ni ya kiwango duni au haifai kwa matumizi.

Maize harvest, Mbola Tanzania

Kuna aina mbalimbali za upotevu wa mazao baada ya kuvuna. Aina ya kwanza ni upotevu wa kiasi cha ubora, upotevu huu unaweza kuupima kwa uzito na ujazo. Hii ni rahisi kuitathmini. Upotevu wa uzito ni ania nyingine ambayo rahisi kupimika. Kukausha kupita kiasi zaidi ya kiwango cha chini (asilimia 13 ya kiasi cha unyevu) ambacho ni salama kwa uhifadhi inaweza kusababisha upungufu wa kipato kutokana na kupoteza uzito wakati wa mauzo.

Upotevu wa ubora, viwango vya ubora vinachukua nafasi kubwa ya sifa na vinahusika na uhalisia kama vile umbo na ukubwa, sifa za kihisia kama vile harufu na ladha, sifa za kikemikali kama vile; kiasi cha virutubisho na usalama pamoja na sifa nyingine kama vile; ubora wa usindikaji.

Uharibifu dhahiri wa mazao kama kuvunjika au kutobolewa kwa nafaka, ambapo inaathiri zaidi ubora na baada ya muda mrefu kusababisha upotevu mahususi. Uharibifu na upotevu vyote vinastahili kupimwa kulingana na uzito na gharama

Upotevu wa moja kwa moja hutokea pale ambapo kupotea kwa chakula kunatokana na kuvuja, udokozi au wizi, kumwagika kutoka  kwenye mifuko, au kuliwa na viumbe waharibifu (wadudu, panya, ndege) ambapo, hasara zisizokuwa za moja kwa moja hutokea kwa kupungua kwa ubora kunakopelekea mnunuzi kukataa kununua mazao..

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *