Kila mwaka, watoto wengi chini ya miaka 5 nchini Tanzania hufa kwa sababu ya lishe duni na chakula. Watoto hawa hawapati chakula chenye vitamini, madini ya iodini na chuma ambayo yanahitajika kwa afya na ukuaji mzuri. Hali hii inasababisha utapiamlo.
Watoto wenye umri wa miezi 6 na zaidi, wapewe chakula cha ziada tofauti-tofauti kwa viwango vidogo mwanzoni na kuongeza kadri wanavyokua.
Vyakula hivi ni pamoja na protini (nyama, maharagwe, samaki, mayai n.k) na vyakula vya nguvu (nafaka – mahindi, mtama, mchele), mboga na matunda.
Upungufu wa virutubisho unashughulikiwa vizuri kupitia mikakati kama bustani za nyumbani na bidhaa ya mifugo wadogo kama kuku wa mayai na mbuzi wa maziwa. Matumizi ya vyakula vya asili kama vile mboga kwenye milo yote kwa viwango vidogo na za mara kwa mara zinaweza kupunguza utapiamlo.
Zingatia lishe Kwa sababu lishe ni muhimu katika ukuaji wa jumla wa mwili na akili kwa watoto, kuna haja ya kuzingatia hasa miaka miwili ya kwanza ya maisha ya mtoto ili kuzuia athari za utapiamlo. Hii inahitaji kushughulika na vihatarishi kuanzia chakula duni, magonjwa hadi upatikanaji duni wa maji safi ya kunywa na usafi wa mazingira.