- Kilimo

Hakikisha unafahamu namna ya kupata mbegu bora kwa mavuno yenye tija

Sambaza chapisho hili

Hasara inayotokana na ununuzi wa mbegu isiyokuwa na ubora ni pamoja na upotevu wa pesa walizotumia kununua mbegu, kuandaa shamba, nguvu kazi iliyotumika kupanda pamoja na muda ambao ungeweza kutumika kwa mambo mengine ya maendeleo.

Mbali na hayo, hali hiyo pia inaashiria hali ya hatari hapo baadaye ambayo inatokana na ukosefu wa mavuno ambayo yangetumika kwa ajili ya chakula pamoja na kipato.

Pamoja na wakulima kulalamika, lakini utafiti unaonesha kuwa hali hii inatokana na makosa wanaofanya wenyewe, kwenye suala zima la uchaguzi wa mbegu na namna ya kupanda mbegu hizo, ingawa pia kuna mbegu ambazo siyo rasmi kutumika kama mbegu.

Zingatia mambo yafuatayo ili upate mbegu sahihi

  • Nunua mbegu zilizozalishwa na wazalishaji wanaotambulika
  • Nunua mbegu kwa wauzaji wanaofahamika na kutambulika kisheria
  • Hakikisha unapata risiti halali kutoka kwa muuzaji
  • Hakikisha muda wa matumizi kwa kuangalia tarehe ya muda wa matumzi kwisha
  • Angalia kibandiko kwenye mfuko endapo mbegu hiyo imepita kwa mkaguzi wa mbegu (TOSCI)
  • Hakikisha mfuko una namba maalumu ya shamba mbegu hiyo ilipozalishwa
  • Hakikisha kifungashio kimefungwa sawa sawa
  • Fuata kanuni sahihi za kilimo
  • Andaa shamba kwa muda unaotakiwa (mwezi 1 kabla ya muda wa kupanda)
  • Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha kabla ya kupanda
  • Hakikisha unaotesha kitaalamu

 

Palizi: Hakikisha shamba linapaliliwa baada ya wiki mbili tangu kupanda. Hii ni lazima hata kama hakujawa na magugu mengi shambani.

Epuka haya:

  • Usinunue mbegu mnadani (sokoni)
  • Usijizalishie mbegu bila kuwa na utaalamu wa uzalishaji mbegu
  • Usichanganye mbegu na mbole. Weka mbolea kisha uifunike
  • Usitumie nafaka ambayo haikuandaliwa kuwa mbegu
  • Epuka kuchukua mbegu kutoka shamba moja kwenda jingine
  • Endapo utakuta kifungashio cha mbegu hakikufungwa sawa sawa, usinunue wala kutumia mbegu hizo.

 

Ni dhahiri kuwa mbegu nyingi hazioti kutokana na wakulima kutokufuata taratibu zinazopaswa, ingawa pia wapo watu wasio waaminifu wanaofungasha nafaka au aina nyingine za mazao ambazo hazikulengwa kuwa mbegu na kuwauzia wakulima.

Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa unafuata kanuni na maelekezo ya wataalamu wa kilimo, ili uweze kupata mavuno bora.

 

Kwa maelezo zaidi juu ya uchaguzi wa mbegu sahihi unaweza kuwasiliana na mtaalamu wa kilimo Bi. Lucy Mvungi kwa simu +255 755 565 621

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *