- Kilimo

Wakulima wazidi kutoa shuhuda

Sambaza chapisho hili

Loseriani Sikayoni:

“Nimepungunza ujinga kwa kiasi kikubwa baada ya kusoma jarida la Mkulima Mbunifu. Nimejua namna ya kufanya kilimo cha mzunguko, natunza mifugo yangu kisasa, faida ni kubwa.”

Ndivyo alivyoanza kusema mzee Loseriani Sikayoni mkulima kutoka kijiji cha Ilkiding’a, mkoa wa Arusha. Kwa miaka mingi, mzee huyu amekuwa akifanya shughuli za kilimo, na maisha yake kwenda vizuri; ikiwa ni pamoja na kutosheleza mahitaji ya familia yake, elimu kwa watoto wake, pamoja na matibabu.

Kilimo kinalipa hasa kikifanywa kwa usahihi+

Mzee huyu ambaye analima mboga mboga, kabichi, karoti, pilipili hoho, nyanya na vitunguu, anasema kuwa wakulima wana uwezo wa kuzalisha na kutosheza soko la Tanzania lakini wamekuwa hawathaminiwi.

“Tuna nguvu ya kuzalisha mazao mengi na chakula cha kutosha, lakini shida moja; serikali haitujali na kutuwekea njia ya kusindika mazao yetu, mazao hayo hayo tunayolima yanaruhusiwa kuingizwa nchini wakati sisi hatuna soko. Nashukuru jarida la Mkulima Mbunifu linaongoza njia sahihi”

Anatoa wito kwa serikali kushirikiana na mashirika binafsi kuthamini na kutoa kipaumbele kwa mazao ya wakulima wa Tanzania kwanza kabla ya kuruhusu mazao mengine kutoka nje kuingizwa nchini wakati mazao yao yanaozea shambani na kupata hasara. Pia wakulima wajiunge kwenye vikundi ili kuwa rahisi kupatiwa huduma, ikiwa ni pamoja na taarifa zinazoweza kuwafanikisha katika kilimo pamoja na masoko.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *