Nilianza kupokea jarida la Mkulima Mbunifu toka mwaka 2012 (Miaka 9 sasa) na kupitia jarida hili nimeweza kujifunza mambo mbalimbali kuhusu kilimo pamoja na ufugaji (Rubia Issa- Kondoa, Dodoma)
Mimi ni mkulima wa alizeti, mahindi na maharage lakini kupitia MkM nimeweza kujifunza kuhusu uchavushaji wa mazao kwa kutumia nyuki hasa alizeti hivyo nikaamua kuwa mfugaji wa nyuki.
Kwa mradi huu wa nyuki wakubwa elimu nimeipata kupitia jarida hili na mpaka sasa nina mizinga hai 69. Pia nafuga kuku kwa ajili ya famila na kuongeza pato.
Mkulima Mbunifu imenifunza pia uzalishaji wa mbogamboga na namna ya kuongeza thamani ya mazao ambapo muda si mrefu nitakuwa msindikaji wa bidhaa mbalimbali.
Najivunia sana kusoma jarida hili na sijutii kwa mafanikio ya kilimo na ufugaji niliyonayo kwasasa nisingeweza kupata popote isipokuwa kupitia jarida hili. Hongera sana Mkulima Mbunifu.