Bustani ya nyumbani ni eneo lililokaribu na nyumbani au jikoni ambalo linaweza kutumika kwa kulima aina mbalimbali za mboga, matunda na viungo vya chakula.
Jinsi ya kuandaa bustani ya gunia
Mahitaji muhimu
- Gunia au mfuko wa salfeti iliotobolewa pande zote
- Kokoto au mawe madogo
- Nguzo au ubao wa 4’ kwa 2’ wenye urefu wa mila moja na nusu
- Mbolea ya samadi au mboji
- Udongo wenye rutuba
- Kopo laujazo wa kilo mbili lenye uwazi pande zote
- Miche ya mbegu ya mboga unayohi- taji kupanda
Maandalizi
- Changanya udongo na mbolea (mboji/mbolea ya asili) kipimo cha 1:2 udongo kipimo cha moja (1) na samadi/mboji mbili (2), kisha anza kujenga magunia.
- Kita nguzo au ubao ardhini kwa umadhubuti
- Visha salfeti/gunia lako na kuifanya nguzo yako kua katikati ya gunia
- Visha kopo na kufanya nguzo iwe kati kati ya kopo
- Jaza kokoto au mawe madogo ndani ya kopo
- Jaza udongo katika mfuko/gunia kufikia kimo cha kopo
- Pandisha kopo juu na endelea kujaza kokoto na kisha udongo kufikia kimo cha kopo
- Endelea kurudia hatua hizi hadi gunia/mfuko wako utakapokuwa umejaa vema
Jinsi ya kupanda
Pima alama za kupandia kwa kuzunguka mfuko katika umbali wa sentimita 15 kutoka tundu hadi tundu kwa aina ya zig zag na kisha toboa tayari kwa kupandikiza.
Panda mboga aina moja kwa kila mfuko
Mfuko huweza kutoa miche 42 hadi 60
Maoni kupitia Facebook
kambalemutumwa@gmail.com
Kuna uwezekano wa kulima kabeji kwa mfumo uo.
Habari, Karibu sana Mkulima Mbunifu. Kuhusu kulima kabeji kwa mtindo wa mfuko huo hapo kwenye picha haitafaa sababu kabichi inakuwa kama tunda na kuning’inia kwake kwenye matundu ya mfuko kutafanya kung’oka na kudondoka. Mtindo huu tumia kwenye mbogamboga zakchuma tu kama chainizi, mnafu, spinach n.k