- Mifugo

Uzalishaji wa minyoo kwa ajili ya kuku, bata na samaki

Sambaza chapisho hili

Minyoo redworms ni chakula kizuri sana kwa kuku, bata na samaki kwani minyoo wana protini nyingi sana na kuku wakipewa au kulishia minyoo wanakua kwa haraka sana na huwafanya kuwa na maumbile makubwa sana (wanakuwa na uzito mkubwa pia).

Kutengeneza minyoo ya chakula ni utaratibu wa kuzalisha minyoo kwa ajili ya kuku, bata na samaki.

Namna ya kuzalisha

  • Chukua mavi ya ng’ombe mapya au mavi ya tumboni kutoka kwa ng’ombe aliyechinjwa
  • Kusanya damudamu, ngozi, mautumbo, nyamanyama
  • Weka vitu vyote kwenye kiroba au gunia
  • Chimba shimo la wastani kisha mwagia maji ndoo kubwa 4 au 5
  • Fukia hilo gunia na mwaga maji ndoo 2 au 3 kubwa, mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 6
  • Baada ya siku 6, fukua na chepe na kisha utakuta minyoo mingi ya kutosha kwa ajili ya chakula cha kuku, bata na samaki.
  • Kadri pia siku zinavyozidi kuongezeka ndivyo minyoo inavyozidi kuzaliana na kuongezeka na kuwa wakubwa.
  • Kwa kufanya hivyo unaweza kufikia uwezo wa kuzalisha ndoo moja kubwa kila baada ya wiki 1 na utakuwa unavuna kwa muda wa miezi miwili na nusu na unaweza ukazalisha tena.

    Minyoo hawa wanaweza kulisha kuku, samaki na bata

Kumbuka; Kwa kufanya hivi utaweza kupunguza gharama za manunuzi ya chakula cha kulishia lakini pia kuku, bata au samaki watakuwa na uzito mkubwa na wenye ubora.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

25 maoni juu ya “Uzalishaji wa minyoo kwa ajili ya kuku, bata na samaki

  1. Tusaidieni oia taarifa za masoko na bei za mazao ya kilimo na mifugo katika mikoa na nchi tofauti duniani kama mnaweza ili tuweze kujua tuzalishe nini kinachouzika kwa being kubwa duniani
    Asante

    1. Karibu sana William, tutajitahidi kwa kadri tuwezavyo tuwaandalie mwenendo wa bei za mazao katika masoko mbalimbali

      1. What if kwa mwenyewe connection ya wa nunuzi akajaribu kuwaweka wazo na kwa mazao/mifugo husika ,on that italeta connection kwa wateja husika

        1. Habari Goodluck
          Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za MkM.

          Ni wazo zuri na kwa kufanya hivyo utafanikiwa kujenga na kuwa na soko la uhakika. Kikubwa ni kujenga uaminifu

          Karibu sana

          1. nataka kupata video ya kutengeneza minyoo kwa chakula cha kuku kibiashara

          2. Habari, karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida letu. Kuhusu video ya minyoo hatuna

            Karibu sana

          3. Hi, welcome to Mkulima Mbunifu and thanks for contacting us. Sure, you will receive it soon via your email address.
            Warmly regards.

      2. Mimi nipo Bukoba mjini Kwaiyo nimependa .Maana Solo spa lipo ,sababu tuko Karibu saana ziwa Viktoria, Ila nina maswali mawili.1.Je unapochanganya huu mchanganyiko unaweka minyoo kidogo au izo takataka ndo zinazalisha minyoo.2 Je kuna mchanganyiko wa vingine ? Ili upate minyoo

        1. Habari,
          Huna haja yakuweka minyoo, ilakama ukiwa nao ukiweka unazalisha kwa haraka sana maana wataendelea kuongezeka .
          Mchanganyiko huu wa taka wenyewe tu unatosha kuzalisha minyoo hii, kikubwa fuata maelekezo kwa ufanisi zaidi

  2. Baada ya kufukua mfuko wa minyoo na kuvuna,unaufukia tena?? Naomba ufafa nuzi zaidi

    1. Hapana, ukishafukua unafukie malighafi zingine mpya, hiyo uliyofukua unalishia kuku. Hivyo ili kupata minyoo mara kwa mara unahitajika kuwa na mzunguko wa uzalishaji

      1. Nauliza kama minyoo iliyozalishwa inafaa kuhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya baadae iwapo idadii ya kuku,Samaki n.k haviendaki na kiasi kilichozalishwa cha hiyo minyoo inakuwa imebaki na kuku wameshiba..je kuhifadhi inafanyika vipi!?.

        1. Habari Eugene

          Tunashukuru sana kwa swali lako zuri
          Kwasasa bado hatujawa na taaluma ya kuhifadhi minyoo kwa ajili ya kulishia baadaye ila tunamshauri Mkulima Kuzalisha minyo mara kwa mara yaani kuzalisha kiwango kinachotosha kulishia kwa kila siku na ikiwa umezalisha wengi basi kuuza kwa wafugaji wengine walio karibu na wewe.

    2. Nashukuru kwa elimu
      Je hayo mautumbo na damu naweka kiasi gani?
      Na je baada ya kufukua ndani ya siku sita nitaendelea kufanyeje ili nivune kwa mienzi miwili kama mlivyoeleza ?

    1. Habari
      Karibu sana Mkulima Mbunifu na tunafurahi kufahamu kuwa wewe ni miongoni mwa wasomaji wa jarida letu hili la kila mwezi.

      Wadudu hao hawana madhara kabisa kiafya kwa kuku kwani ni chakula ambacho ni chanzo cha protini kwa wingi ni kama binadamu kula kukua au samaki.

      Karibu sana

  3. Asante kwa elimu nzuri
    Malighafi kwa ajili ya kupata hiyo minyoo lazima itokane na ng’ombe pekee yake? Napenda kujua ukubwa wa shimo kwa vipimo kama inawezekana. Asante endeleeni kutuelimisha maana elimu haina mwisho

    1. Habari Peter
      Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kutufuatilia na kusoma makala zetu. Kuhusu minyoo hii, si lazima watokane na ng’ombe mara nyingi mbolea au muozo wa aina yeyote huweza kuwa chanzo cha kuwapata, ila kwasababu unalenga kuwalisha kuku kama chakula ni vyema ukatumia njia tuliyofundisha hapo ili kuweza kuwazalisha kwa wingi na kwa haraka zaidi.

      Kuhusu ukubwa wa shimo, halina vipimo maalumu kwani kinachotakiwa ni ili tu kupata sehemu pa kuzalishia

    1. Habrai, Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala zetu.

      Ni vyema kutumia malighafi zote zilizoorodheshwa kwani bila kuwa nazo huwezi kupata au kuzalisha minyoo

  4. Naomba kujua je nikitumia kinyesi cha mbuzi kutoka kwenye utumbo siwezi kuzalisha hao minyoo

  5. Ni mavi ya ngombe tu yanayofaa kwa uzalishaj wa minyoo( hakuna mbadala)?
    Na nilazima yawe mavi mabichi ( mapya) nikichukuwa makavu nikayaroweka na maji baadae nikafata njia ulizozieleza hapo,hayatofaaa???
    Hata nikichukuwa ujazo wa kiroba cha kilo 5 , nitaweza kupata mavuno ya miez miwili au kuna ujazo maalum ili kupata mavuno ya muda mrefu???
    Wakat wakuvuna, ninafukuwa tu shimo nikawaacha wakule wenyewe au lazima niwatolee nje???
    Nikuku rika lote wanakula hii minyoo au kuna rika maalum?

    1. Habari, karibu mkulima mbunifu na asante kwa swali lako.

      Ukisoma hiyo makala vizuri tumejarobu kueleza vyema na kwa urahisi kabisa. Mavi au kinyesi ni cha ng’ombe na tumeeleza kabisa kuwa ikiwezekana chukua kinyesi kipya kabisa. Kadri unavyozalisha kwa wingi ndip[o utakapopata minyoo wengi, huwezi ukazalisha kidogo ukategemea kupata wengi lakini pia na wakati huohuo ukiwa unatumia kulishia. Hivyo kama unataka minyoo wengi kwa wakati mmoja tumia malighafi nyingi kuzalisha kwa wakati mmoja.

      Uvunaji unategemea wewe mwenyewe ila ni vyema ukatoa kiasi fulani ukalishia kuku na si kuwaacha kuku wakafukua kwenye malighafi wenyewe.

      Kuku wa aina zote na rila zote wanaweza kulishwa isipokuwa ni vyema kuwa makini na vifaranga sababu wanaweza kumeza na kukabwa na mnyoo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *