- Mifugo

Ulishaji sahihi na uangalizi wa karibu kwa mtamba anayekua ni muhimu

Sambaza chapisho hili

Kwa ajili ya kupata mtamba anayeweza kukupatia ndama kila mwaka ulishaji ni muhimu.

Tengeneza mzunguko wa siku 365

Inawezekana kuwa na mzunguko wa kupata ndama na uzalishaji katika kipindi chote cha mwaka. Hii inamaanisha kwambwa ng’ombe wako anaweza kukupatia ndama kila mwaka, (siku 365).

Ng’ombe ana uwezo wa kuwa kwenye joto kila baada ya siku 40-60 tangu kuzaa. Ili kumuwezesha kuwa na ndama katika kipindi kinachofanana cha mwaka, mpe nafasi ya siku 80-90 za kupumzika kabla ya kumpandisha tena.

Fanikisha na uimarishe mzunguko wa uzalishaji wa siku 365:

  • Kuangalia afya ya mifugo wako mara kwa mara ili kuwa na uhakika kuwa viungo vyake vya uzazi viko katika hali ya kuwezesha kuzalisha. Endapo kuna maambukizi yanaweza kuathiri ubebaji mimba kwa mifugo yako.
  • Umpandishe ng’ombe ndani ya siku 100 toka alipo zaa.
  • Kuwa na utaratibu wa mara kwa mara wa kumwangalia ng’ombe kama yupo kwenye joto, inapotokea apandishwe mara moja.
  • Ng’ombe akaguliwe baada ya miezi mitatu ili kuwa na uhakika kama alipopandishwa alishika mimba au la, endapo hakushika mimba inabidi aangaliwe kwa karibu kufahamu ni lini anaweza kupandishwa tena, na hatua hiyo irudiwe kwa uangalifu. Inawezekana kukawa na muda mrefu zaidi wa uzalishaji endapo ng’ombe hatakaguliwa kama ana mimba baada ya kipindi hicho.
  • Kamua ng’ombe kwa siku 365 kisha uache na umuandae kwa ajili ya kuzaa tena. Siku sitini (60) za kuacha kukamua zinatosha.
  • Fuata utaratibu mzuri wa lishe na virutubisho ambao utawezesha ng’ombe kujenga mwili vizuri na kuwa na mzunguko mzuri ambao utamuwezesha ng’ombe kukabiliana na changamoto katika kipindi cha uzalishaji wa hali ya juu (ubebaji mimba na uzalishaji wa maziwa). Hakikisha unamlisha ng’ombe mlo kamili (kiwango sahihi cha virutubisho na majani). Weka mikakati thabiti itakayokuwezesha kuwa na uzalishaji mzuri na afya kwa mifugo yako. Jambo muhimu ni kuwa na vyakula vya kutia nguvu kwa ajili ya ng’ombe wako baada ya kuzaa.
  • Kumbuka kumtumia mtaalamu wa kupandikiza ng’ombe anae aminika na alie idhinishwa. Hautakiwi kulipia aina flani ya mbegu na kupandikizwa aina nyingine, hili linaweza kutokea endapo hautamtumia mtaalamu mwenye uhakika.

Mfugaji ni lazima azingatie haya ili kuwa na mitamba yenye afya inapatiwa lishe duni.

Mitamba haiwezi kukua kwa haraka endapo atapatiwa lishe duni. Ndama mwenye lishe duni atachelewa kubeba mimba na pia kiwango chake cha uzalishaji wa maziwa kitakuwa kidogo.

  • Ulishaji wa kupindukia wa vyakula vya kutia nguvu, husababisha ng’ombe kunenepa na kusababisha mrundikano wa mafuta kwenye matezi yanayozalisha maziwa hivyo kusababisha uzalishaji mdogo wa maziwa.
  • Lishe duni kwa mtamba husababisha kudumaa, umbo dogo husababisha ugumu wakati wa kuzaa. Ulishaji uliopindukia kwa mtamba pia husababisha ugumu wa kufunguka kwa njia ya uzazi wakati wa kuzaa hivyo kusababisha matatizo na ugumu wakati wa kuzaa pia.
  • Ukubwa wa mtamba hutoa mwelekeo wa kiwango cha maziwa kitakachozalishwa. Kwa mfano, kama mfugaji ana mitamba ambao ni pacha, mwenye umbo kubwa anategemewa kuzalisha maziwa mengi zaidi kuliko mwenye umbo dogo.
  • Ulishaji wa vyakula vya kutia nguvu zaidi ya protini hupelekea kuwa na mtamba mfupi ila mnene. Kwa upande mwingine ulishaji wa protini nyingi husababisha kuwa na mtamba mrefu lakini mwembamba. Sileji ya mahindi ni moja ya malisho bora
  • Utengenezaji wa sileji ni moja ya mbinu za kuhifadhi malisho kwa njia ya uvundikaji. Malighafi zilizozoeleka katika utengenezaji wa sileji ni pamoja na matete, majani ya mahindi, mtama, ngano, na majani ya miwa.

Inapendekezwa kuwa mifuko inayotengenezea sileji ijazwe karibu na sehemu ya kuhifadhia, hii ni  kwa sababu sileji ni nzito na ni vigumu kuhamisha ikishajazwa sileji.

Katakata malighafi zilizo nyauka kisha yanyunyizie maji yaliyochanganywa na molasesi (Kwa kila gunia moja tumia lita 1 ya molasesi iliyochanganywa na maji lita 2-3). Hii ni muhimu kwa malighafi zenye kiwango kidogo cha sukari kama vile matete. Pumba za mahindi au unga wa muhogo unaweza kuongezwa kwenye mchanganyiko huo ili kuongeza virutubisho vya kutia nguvu, na majani ya miti tofauti kama njia ya kuongeza protini.

Jaza majani kwenye mfuko wa nailoni kiasi cha kukaribia kujaa, yashindilie  na ufunge vizuri. Kwa kawaida majani haya huiva baada ya siku 21. Ng’ombe wa gredi anaweza kula mpaka kiasi cha kilo 40 za sileji kwa siku. Kwa ng’ombe anaezalisha maziwa zaidi ya lita 8, aongezewe kilo 1 ya chakula maalum cha ng’ombe wa maziwa kiasi cha kilo 1 kwa kila kilo 1.5 za maziwa.Ili kuepuka ladha mbaya kwenye maziwa, lisha ng’ombe kwa kutumia sileji baada ya kukamua wakati wa asubuhi au saa tatu kabla ya kukamua wakati wa jioni.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *