- Mifugo

Tengeneza chakula kwa ajili ya nguruwe kwa kutumia comfrei na upupu

Sambaza chapisho hili

Ni kwa namna gani ninaweza kutengeneza chakula cha nguruwe kwa njia kutumia comfrei na upupu?

Resheni ya chakula inahusiana moja kwa moja na ulishaji. Hili ni jumuiko la aina mbalimbali ya vyakula vinavyotumika kwa malisho, ikionesha ni kiasi gani cha kila aina ya lishe iliyopo kimetumika ili kuwa na chakula bora.

Hii inamaanisha kuwa resheni inakamilika inapokuwa na aina zote za virutubisho vinavyohitajika katika kila mlo mmoja, ambapo ubora wa resheni pia unategemeana na ubora wa malisho yaliyotumika kutengeneza resheni hiyo.

Kwenye resheni yoyote, kuna asilimia fulani ya malisho ambayo hutumika ili kukamilisha resheni hiyo inayohitajika. Mchanganyiko kamili wa resheni hiyo hukamilisha asilimia mia moja (100%) ya mahitaji halisi. Kinachobainisha mchango wa virutubisho kwa kila resheni ni asilimia ya virutubisho kwa kila aina ya malisho na virutubisho vilivyotumika katika resheni hiyo.

Resheni ya mfugaji Resheni inayotengenezwa na mfugaji mwenyewe, inaweza kusaidia kupunguza gharama za ulishaji wa nguruwe. Hata hivyo, ulishaji kwa kutumia mchanganyiko fulani ni lazima uzingatiwe, pamoja na mchanganuo wa sampuli zinazotumika ni lazima kuzingatiwa mara kwa mara.

Comfrei na upupu usiowasha, unaweza kutumika badala ya vyakula vya kununua kama ifuatavyo:

  • Comfrei 20%, upupu usiowasha 20%, nafaka 60%.

Matayarisho ya awali ya upupu usiowasha

  • Loweka upupu usiowasha kwenye maji baridi na uache usiku mzima.
  • Osha upupu huo kwa maji safi siku inayofuata.
  • Ushemshe kwa muda wa saa moja.
  • Suuza kwa kutumia maji baridi.
  • Kausha kwenye jua.
  • Saga kwa kutumia mashine au njia nyingine ambayo ni rahisi kwako.
  • Changanya 25% ya unga wa upupu usiowasha na 75% ya nafaka.

Kumbuika: Vyakula vya nguruwe vinavyonunuliwa 20%, malisho unayolima shambani 80%.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *