Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi mwaka huu wa 2025 itaendesha nchi nzima zoezi la uchanjaji wa Ng’ombe dhidi ya Ugonjwa wa Homa ya Mapafu (CBPP), Mbuzi na Kondoo dhidi ya Ugonjwa wa Sotoka (PPR) na Kuku dhidi ya Ugonjwa wa Mdondo/ Kideri (Newcastle disease)
Gharama ya chanjo kwa Ng’ombe mmoja ni shilingi mia tano (500/=), Mbuzi/Kondoo mmoja ni shilingi mia tatu (300/=). Kuku watachanjwa BURE
Katika zoezi hili la chanjo, majukumu ya mfugaji ni kama ifuatavyo:-
- Kushiriki katika kuandaa eneo na miundombinu ya kutolea huduma ya chanjo.
- Kushirikiana na vyama vya wafugaji na viongozi wa vijiji au mitaa kuhamasisha umuhimu wa chanjo kwa wafugaji wengine katika zoezi la chanjo.
- Kupeleka mifugo kwenye vituo vya chanjo kulingana na ratiba ya chanjo.
- Kulipia gharama za chanjo kama inavyoelekezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ama uongozi wa Halmashauri kwa maeneo husika.
- Kutunza daftari la kumbukumbu za chanjo zinazotolewa katika mifugo yake kwa lengo la kusaidia ufuatiliaji wa kiwango cha uchanjaji, ubora na watoa
Maoni kupitia Facebook