- Mifugo

Namna ya kuzuia ugonjwa wa ndigana kali

Sambaza chapisho hili
  • Mfugaji ajitahidi kuogesha wanyama wake vizuri walau mara moja kila wiki kwa kutumia dawa ya kuua kupe.
  • Ogesha kwa kutumia dawa zinazozuia kupe na mbung’o katika eneo unalofugia. Kwa mfano unaweza kutumia; Tristix, Tixfix, Ciberdip, Paranex, Alfanex, Steladone, Dominex na kadhalika.
  • Epuka kuchunga mifugo katika maeneo yenye kupe au mbung’o wengi. Ikibidi chunga kwa mzunguko (rotational grazing) katika eneo  lako ili kuzuia kuzaliana kwa kupe.
  • Kuchunguza ugonjwa: Uchunguzi hufanyika kwa kuangalia dalili za ugonjwa. Endapo mnyama hana dalili, chukua sampuli ya damu na kuipeleka maabara. Itachunguzwa kwa darubini ili kuhakikisha na kujiridhisha juu ya uwepo wa vimelea.

Tiba

Tumia dawa ya Oxytetracycline (OTC) ya sindano kiwango cha 5-10mg kwa kilo ya uzito wa mnyama au soma maelekezo ya mtengenezaji wa dawa husika. Wanyama waliofunga choo wanyweshwe mafuta ya kupikia ili kulainisha utumbo.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *