Utunzaji wa ndama mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya maziwa.
Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na;
- Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tinture of Iodine) mara baada ya kuzaliwa.
- Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara baada ya kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Aidha, aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.
Endapo jike aliyezaa amekufa au hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo;
- Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
- Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
- Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oil).
- Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3 na yai moja bichi.
Koroga mchanganyiko huo, weka katika chupa safi na ndama anyweshwe kabla haujaopoa. Ndama anyweshwe mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3 mfululizo na kila mara mchanganyiko uwe mpya.
Wakati wa kunywesha chupa iwekwe juu ya kidogo ili asipaliwe.
- Endapo ndama hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama anyweshwe maziwa kwa njia ya chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa.
- Ndama aendelee kunyweshwa maziwa kwa kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali na. 1
- Ndama aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakti wote kuanzia wiki ya 2 baada ya kuzaliwa.
- Ndama aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi 3. Mfugaji ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya nzuri.
Matunzo mengine ya ndani ni pamoja na;
- Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana na kuharibu Ngozi.
- Kukata chuchu za ziada kwa ndama jike.
- Kuhasi ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao hawatahitajika kwa ajili kuendeleza kizazi ili wakue hawatajika kwa ajili ya kuendelea kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
- Kuweka alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa ajili ya urahisi wa udhiti wa umiliki na utunzaji kumkukumbu.
- Kuwapatia kinga dhidi ya maabukizi na tiba ya magonjwa wanapougua. Huduma hizi zifanyike chini ya maelekezo ya mtaalam wa mifugo.
Utunzaji wa ndama baada ya kuachishwa maziwa hadi kupevuka (miezi – 18).
Ndama baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na chakula mchanganyiko kuanzia kilo 2.4 kwa siku kutegemea umri wake.
Ndama wanapofikia umri wa miezi 18 wachaguliwe wanaofaa kuendeleza kizazi, wasio na sifa nzuri waondolewe katika kundi.
Utunzaji wa mtamba
Mtamba ni ng’ombe jike aliyefisha umri wa kupandwa (wastani wa miezi 18) hadi anapozaa kwa mara ya kwanza. Ni muhimu kutunza vizuri mtamba ili kupata kundi bora la ng’ombe. Miezi 3 kabla ya kupandishwa mtamba apatiwe;
- Malisho bora.
- Maji ya kutosha.
- Madini mchanganyiko.
- Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji na kuongeza uzito wa mwili.
Utunzaji wa ng’ombe wakubwa
Kundi hili linajumuisha ng’ombe wenye mimba, wanaokamuliwa na madume. Mfugaji anapaswa kutunza vizuri ng’ombe