Kupe ni wadudu wanaoonekana kuwa ni wadogo lakini wanaweza kusababisha kushuka kwa uchumi wa wafugaji kwa kiwango cha juu endapo hawatadhibitiwa kwa wakati.
Pamoja na kuwepo kwa aina mbalimbali za kupe, kupe wa rangi ya kahawia ni wabaya zaidi. Hii ni kwa sababu kupe wanabeba vimelea vinavyosababisha homa ya ndigana (East Coast Fever). Kupe wanaonekana kuwa wababe wa maisha kutokana na sababu kuwa kitendo cha kuchoma maficho yao bado haisadii kuwatokomeza, kwani wadudu hawa huweza kujichimbia ardhini urefu wa sentimeta 20 na wakaishi kwa muda wa miaka miwili bila kufa na bila kula chochote.
Mbali na hayo, kupe huwa sugu wa madawa kwa haraka hivyo wafugaji wanatakiwa kubadili madawa kila wakati ili kuweza kuwadhibiti. Mbaya zaidi, wauzaji wengi wa madawa ya kuogesha mifugo hawako tayari kuwaeleza wafugaji kuhusu uwezo wa dawa hizo, jambo ambalo wafugaji wengi wamekuwa wakichanganya dawa kupita kiasi kwa lengo la kupunguza gharama za manunuzi na hivyo kuua nguvu ya dawa.
Kemikali zilizo katika kiwango kizuri cha kutibu ni zile zinazotokana na pareto na zinazofanya kazi kwa haraka. Hutumiwa kama dipu au kupulizia kwa wanyama kwa kutumia bomba la mkono.
Madawa haya huwa katika kimiminika kama mafuta ya maji ambapo mfugaji atatakiwa kumpaka ng’ombe mgongoni. Mafuta hayo husambaa katika mwili wote wa mnyama hivyo kumkinga kushambuliwa na kupe.
Ingawa mzunguko wa upuliziaji wa madawa haya hufanyika kila wiki, gharama za udhibiti wa vipimo uko juu sana kwa wakulima wadogo. Kwa mfano, kupiga dipu kwa wiki ni shilingi 1,500 hadi 2,000 kwa ng’ombe mmoja. Hii ni kwa sababu serikali Hizi ni aina tatu za kupe ambao hushambulia mifugo, ngómbe huathiriwa zaidi.
Kupe hupendelea sehemu zilizojificha kwenye mwili wa mnyama. Baadhi ya watu wanaofanya shughuli hizo wamekuwa wakidanganya wafugaji kutokana na sababu kuwa hawanyunyizii dawa sahihi na kwa kiwango cha kutosha mifugo, jambo ambalo linasababisha kupe kutokufa na kuendelea kuisumbua mifugo.
Kwa kuweka uzio na kuwa na mazingira mazuri kwa ufugaji, wakulima wanaweza kujiepusha ama kupunguza uharibifu unaosababishwa na kupe huku wakizingatia kufuga kwa kiasi. Pia, kuwaruhusu kuku kutembea karibu na ng’ombe au katika maeneo ya ufugaji, kutasaidia kupunguza wingi wa kupe kwani kuku hula kupe.
Njia za kiasili za kuwadhibiti kupe
Diatomite: Huu ni unga mweupe wa madini ya asili diatomaceous ambayo hutumika katika udhibiti wa kupe. Chembechembe zake kali husambaa katika mwili wote wa mdudu na kunyonya majimaji yote mwilini. Kukosekana kwa maji mwilini husababisha mdudu kufa. Unga huo husambaa katika mwili wote na kunyonya maji, na ni vigumu kwa mdudu kujitengenezea kinga kwa wakati huo na ndiyo maana hufa.
Pareto: Chukua gramu 250 za maua yaliyokauka ya pareto, weka kiasi kidogo cha maji kisha tia kwenye kinu na utwanga. Baada ya kumaliza, weka maji hadi kufikia lita 10, chemsha kwa dakika 20. Epua na uiache kwa muda wa saa 12, kisha nyunyizia mifugo. Pia unaweza kuchukua gramu 250 za maua ya pareto yaliyokauka, weka maji lita kumi, hifadhi kwenye chumba chenye giza na uache kwa muda wa saa 12, baada ya hapo itakuwa tayari kwa kuitibu mifugo.
Tumbaku: Chukua kilo moja ya majani mabichi ya tumbaku, tumbukiza katika maji lita 10 kisha iache kwa muda wa dakika tatu. Tumia kitambaa safi kumpaka ng’ombe. Lita 5 zinatosha kwa ng’ombe mmoja.