Mkulima Mbunifu ni huduma ya habari za kilimo inayowalenga wakulima wadogo kupitia jarida la kila mwezi, redio, na huduma nyingine kwa njia ya mtandao.
Kilimo nchini Tanzania ni tegemeo kubwa la kiuchumi kwa watu wengi. Kilimo kinachangia zaidi ya asilimia 50% ya Pato la Taifa na kinaajiri karibu asilimia 80% ya idadi ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi.
Wakulima wadogowadogo wanaendelea kutumia njia za jadi kupata na kupashana habari na maarifa ambayo hayajitoshelezi na hayatoshi kukabiliana na changamoto za sasa zinazowakabili wakulima hawa.
Jarida la Mkulima Mbunifu linalotoa taarifa za kilimo na ufugaji kwa wakulima. Linachapishwa kila miezi na kusambazwa kwa vikundi vya wakulima waliohitaji.
Mpaka sasa wakulima wengi wanafaidika na machapisho haya na kuweza kuongeza uzalishaji, pamoja na kuongeza mbinu za utunzaji wa mazingira.
Malengo yetu ni kuwa na machapisho endelevu yenye taarifa sahihi na za kutegemewa juu ya uhusiano wa mimea, wanyama na binadamu, ambayo yanaweza kutumiwa na wakulima Afrika ya mashariki. Kwa kuongezea, muunganiko wa machapisho haya kupitia MkM yataweza kufanya uwepo na ongezeko la ufahamu miongoni mwa watu, taasisi na watunga sera wenye lengo linalofanana.
Wasomaji na wasikilizaji wetu ni jamii ya wakulima ambao wana nia ya kujifunza zaidi juu ya kilimo endelevu na uhusiano kati ya mimea, wanyama, binadamu na mazingira. Hivyo tunachapisha nakala za MkM kila mwezi na kusambaza kwa vikundi vya wakulima nchini Tanzania.
Washirika wetu www.infonet-biovision.org ni tovuti maktaba ambayo wakulima wanaweza kutegemea kwa kiasi kikubwa kupata taarifa kuhusiana na uhusiano wa mimea, wanyama, binadamu na mazingira, pamoja na wadudu na maambukizi ya magonjwa.
Lengo hapa ni kutoa elimu inayoendana na wakati juu ya udhibiti wa magonjwa ya wanyama na binadamu, pamoja na mbinu za kuongeza uzalishaji wa chakula Afrika Mashariki. Matumizi ya mbinu hizo yanawekwa katika jukwaa huru yakilenga mahitaji ya wakulima wa ndani, kilimo na washauri wa afya kuweza kupata taarifa sahihi kwa haraka zaidi.
Jarida hili linatayarishwa kila mwezi na Mkulima Mbunifu, Arusha, ni mojawapo ya mradi wa mawasiliano ya wakulima (Farmer Communication Program – FCP) unaotekelezwa na Biovision Africa Trust (BvAT) – https://biovisionafricatrust.org/ kwa ushirikiano na Sustainable Agriculture Tanzania (SAT – https://kilimo.org). Jarida hili linafadhiliwa na Biovision Foundation (www.biovision.ch).
Kwa maoni au maswali tafadhali wasiliana nasi kupitia;
- Namba ya simu: 0717 266007, 0785 133 005
- Barua pepe: info@mkulimambunifu.org
Washirika wetu
Biovision Foundation
Sustainable Agriculture Tanzania
Biovision Africa Trust