Safari ya kuongeza thamani nyama ya mifugo huanzia shambani kwa usimamizi wa ufugaji na uzalishaji. Lishe bora ni muhimu kwa wa ufugaji wa mifugo wa nyama, hivyo, nyama nzuri huanza na lishe bora. Malisho ya hali ya juu yasiyokuwa na vimelea vinavyoweza kusababisha magonjwa na kemikali hatari yanakidhi mahitaji ya lishe ya mnyama. Hii itahakikisha mnyama anapochinjwa anatoa nyama laini isiyokuwa na mafuta mingi. Na hii hupendwa na walaji wengi.
Ukaushaji wa nyama
Nyama inauzwa nchini kwa njia mbalimbali na kwa urahisi ili kukidhi mahitaji ya walaji. Nyama huwa na thamani kubwa ya kibayolojia na huchangia katika kupambana na utapiamlo na upungufu wa protini ambayo ni shida kuu mbili katika nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Tanzania.
Kutokana na hilo, msisitizo mkubwa unawekwa katika kuimarisha teknolojia zinazofaa za kutengeneza bidhaa za nyama ili kukidhi hali ya watu, hasa walio maeneo ya vijijini.
Matumizi ya nyama katika utengenezaji wa bidhaa inasisitizwa kwa sababu yana ubora wa virutubishi kama vile protini ya hali ya juu, vitamini, madini mengine vya umuhimu mkubwa kwa mwili wa binadamu.
Kuhifadhi nyama
Kukausha nyama kutumia joto la asili, unyevu na mzunguko wa hewa, ikiwa ni pamoja na miale ya jua ya moja kwa moja ni njia ya tangu jadi ya kuhifadhi nyama. Inajumuisha kupunguza maji iliomo kwenye vipande vya nyama vilivyokatwa-katwa ili kuruhusu kukauka kwa utaratibu.
- Nyama isiyokuwa na mafuta inafaa kwa kukausha na ikiwezekana iwe nyama ya mnyama wa umri wa kati na aliye katika hali nzuri.
- Kata nyama katika vipande virefu vinavyofanana na inayofuata nyuzi za misuli. Urefu wa vipande unaweza kutofautiana, ingawa haipaswi kuwa chini ya sentimita 20 na isizidi senstimita 70. Nyama iliyokatwa vipande vifupi inahitaji muda mwingi zaidi kuyaweka pamoja kuliko ile iliyokatwa vipande virefu. Lakini, vipande ambavyo ni virefu sana vinaweza kuvunjika kwa sababu ya uzito wake.
- Unene wa vipande huamua muda wa mchakato wa kukausha. Kwa kuwa vipande vinene huchukua muda zaidi kukauka kuliko vile vyembamba, ni muhimu kwamba vipande vya kuwekwa kwenye kundi moja ziwe zinafana kwa urefu na unene.
- Weka vipande ndani ya maji ya chumvi kwa muda wa dakika 5 (ndani ya saa 5 baada ya kuchinja) kisha ondoa maji kwa kutumia chujio. Chumvi huzuia ukuaji wa vijidudu na kuwazuia nzi.
- Tumia waya ya chuma usioshika kutu kuzishikilia vipande vya nyama. Simamisha au ning’iniza kila kipande cha nyama kutoka mwisho ili kuhakikisha mzunguko wa hewa na kukausha kwa haraka. Epuka vipande vya nyama kugusana kwa kuwa maeneo yaliyogusana yatabaki na unyevu kwa muda mrefu, na kuleta mazingira mazuri ya uharibifu, bakteria na inzi. Vipande vya nyama vilivyofungwa kwenye waya wa chuma vinaweza kusimamishwa kwenye mbao, Kamba au waya.
- Ning’iniza kwenye nguzo iliyotengenezwa kwa mbao au chuma. Kausha kwa muda wa siku 4 hadi 5 na baada ya kipindi hiki, nyama iko tayari kwa matumizi, ufungashaji au usafirishaji.
- Wakati wa ukavu, nyama iliyokatwa vipande vyenye umbo hizi mbili ndio hufaa zaidi kwa ukaushaji wa asili: vipande viliyokatwa mstatili wa sentimita 1 x 1 na vipande vilivyokatwa umbo la jani wa sentimita 0.5 x takribani sentimita 3, 4 au 5.
Viwango vya ubora wa nyama iliyokaushwa
Kukausha nyama inachukua siku nne hadi tano. Baada ya kipindi hiki nyama iliyokaushwa iko tayari kwa matumizi na inaweza kufungwa, kuhifadhiwa au kusafirishwa. Ni vyema kuhakikisha kwamba bidhaa hii inafikia vigezo vifuatavyo vya ubora.
- Muonekano wa nyama kavu lazima iwe ya usawa iwezekanavyo. Uwepo wa mikunjo ni ishara kwamba nyama imekauka vizuri. Rangi yake isiwe nyekundu ya damu bali nyekundu yenye weusi kidogo.
- Nyama iliyokaushwa inapaswa kuwa na ladha ya chumvi kidogo, hasa kama imekaushwa asili bila viungo. Harufu mbaya haipaswi kutokea. Nyama iliyokaushwa iliyo na mafuta mengi haipaswi kuhifadhiwa kwa muda mrefu, lakini itumike haraka iwezekanavyo ili isiharibike.
- Nyama iliyokaushwa lazima ichunguzwe mara kwa mara ili kubaini harufu inayohusiana na kuharibika, ambayo ni matokeo ya utayarishaji usio sahihi au ukaushaji wa nyama. Nyama iliyo na dalili za kuharibika lazima ichaguliwe na kutupwa.
Soseji
Soseji ni aina ya bidhaa ya nyama ambayo kwa kawaida hutengenezwa kutokana na nyama ya kusagwa mara nyingi nyama ya nguruwe, nyama ya ng’ombe, au kuku, pamoja na chumvi, viungo na ladha nyinginezo.
Viungo vingine, kama vile nafaka au mkate vinaweza kujumuishwa kama vichungi au virefusho.