Kuku wa kienyeji nao wanahitaji kupata chanjo ya magonjwa na kwa utaratibu unaofaa.
Ugonjwa | Jinsi ya kuudhibiti |
Mdondo/kideri (Newcastle disease) | Kama tete lilichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki tatu za kwanza za maisha yao.
Wachanje vifaranga hawa dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.
Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku ya 3 mara baada ya kuanguliwa, rudia wafikishapo wiki 3, kisha uchanje kila baada ya miezi mitatu (3). |
Ndui ya kuku | Vifaranga wapewe chanjo ya kuzuia ndui wafikishapo umri wa mwezi mmoja. |
Ukosefu wa vitamini A | Watafutie kuku majani mabichi au hata machicha mara kwa mara. Kama hakuna majani wape vitamin ya kuku kutoka dukani kama ziada. |
Ugonjwa wa kuharisha damu (coccidiosis) | Safisha banda kila siku na hakikisha hakuna unyevu sakafuni. Wape vifaranga dawa ya kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wakishapo umri wa siku 7 tokea waanguliwe. |
Viroboto, chawa na utitiri | Mwaga majivu katika banda na hasa kwenye viota vya kutagia ili kukinga wadudu. Tumia dawa za dukani mfano; Akheri powder au sevin dust kumwagia kuku mwilini na katika mazingira. Paka mafuta ya taa kwa kutumia unyoya wa kuku kwenye viroboto vunavyoonekana. |
Minyoo | Wape vifaranga dawa ya minyoo mara wafikishapo umri wa miezi miwili kisha rudia kila baada ya miezi mitatu. |
Maoni kupitia Facebook
Napenda kujifunza juu ya huduma wa ufugaji wa kienyeji
Karibu Mkulima Mbunifu, Ungependa kujifunza kuhusu ufugaji wa mifugo gani?