- Kilimo

Tumia mitego kunasa wadudu wkenye matunda na mboga

Sambaza chapisho hili

Kutengeneza mitego mwenyewe

Ili kutengeneza mtego wa kunata, sambaza petroleum jeli au oili chafu kwenye mbao laini, iliyopakwa rangi ya njano (ukubwa wa sm 30 kwa sm 30). Weka mitego karibu na mimea lakini ikae mbali kidogo kutoka kwenye shina ili kuzuia majani yanayoanguka yasinase kwenye bodi.

Chukua tahadhari kwamba rangi ya njano huvutia aina nyingi za wadudu, wakiwemo wadudu rafiki, kwa hiyo tumia mitego ya njano pale tu inapokuwa ni lazima.

Mitego kwa ajili ya inzi wa nyumbani na inzi wa matunda

Inzi wa matunda na inzi wa nyumbani huvutiwa na juisi ya matunda inayochacha. Sehemu ya juu ya chupa ya plastiki inaweza kukatwa kabisa na kugeuzwa.

Maji kidogo yenye sukari au asali yanaweza kupakwa kwenye ukingo wa chupa ili kuwavutia inzi zaidi, ambao baada ya hapo huingia kwenye chupa yenye juisi ya matunda inayochacha na kunaswa.

Mitego ya inzi wa matunda inaweza kutengenezwa popote kwa kutumia jagi la kawaida na kontena au chupa za plastiki zilizotobolewa matundu. Mitego hii inaweza kutumika na mitego ya chakula kama vile proteni haidrolisate, hamira au juisi tamu au inayochacha.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *