- Kilimo, Kilimo Biashara, Masoko, Mifugo

Soko la mbogamboga hutokana na uzalishaji

Sambaza chapisho hili

Soko ni mahali au njia ambayo muuzaji na mnunuzi hukutana na kubadilishana mali au huduma. Ni fursa ya kuuza na kununua.

Kwa kawaida tunapozungumzia soko, tunagusia mambo kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na ukubwa wake, yaani wingi wa wauzaji na wanunuzi katika soko husika, ushindani, washindani, bidhaa na bei zake, changamoto, pamoja na mabadiliko yanayotegemewa.

Kwa upande mwingine, tunaweza kuzungumzia soko katika mgawanyo wa makundi na tafsiri tofauti kama vile:

• Soko ni mchanganyiko wa shughuli ambazo hufanywa na mjasiriamali

katika kuuza mali/mazao yanayotarajiwa na manunuzi ya wateja/ wadau

• Ni mchakato wa mategemeo ya matakwa ya wateja/wadau na kutafuta njia ya kuridhiana na kupata faida

• Ni mahali pa kumleta mteja na kumridhisha kwa faida

Upembuzi yakinifu wa masoko hugusa yafuatayo:

• Mazao

• Bei

• Mahali

• Na kutangaza bidhaa

Hizi ndizo shabaha za masoko

Ili kupata soko lenye uhakika na faida kwa wakulima na wafugaji, ni lazima wakahakikishe wanazingatia mambo muhimu yafuatayo. 

Mazao

• Mazao yawe na ubora unaokubalika na soko

• Yawe na uwezo wa kukaa muda mrefu kabla ya kutumika yaani uhai wake ghalani

• Jina la zao unalozalisha

• Jinsi ya kufungasha zao hilo (mboga/ matunda) katika hali ya ubora na

salama.

• Aina gani ya mbogamboga/matunda unayouza na je, yanaweza kuuzika

• Mara baada ya kuuza ni huduma zipi zinatarajiwa au kuhitajika.

• Kuna makubaliano gani unaweza kutoa?

Bei

• Ni muhimu kufahamu kuwa utauza mazao yako kwa bei gani

• Je, zao lako litauzwa kwa bei tofauti kwenye masoko mengine?

• Usambazaji utakuwa mkubwa kiasi gani

• Utatumia usafiri wa aina ganibaiskeli, pikipiki, gari, kichwa au aina gani?

• Je, kuna vituo vya usambazaji

• Jinsi ya kupanga maeneo ya mauzo

• Ni kiasi gani cha mbogamboga na matunda unaweza kutoa kwa wanunuzi wako

• Ni wapi utahifadhia mazao yako

Kutangaza bidhaa

Nyanja hii ni muhimu sana kwa biashara yako pia. Hii ni kwa sababu ndiyo inayofanya uweze kufahamika vizuri na bidhaa yako kupata wanunuzi wa kutosha. Fahamu ni njia ipi utatumia kati ya hizi:

• Kuuza wewe binafsi

• Kuweka mabango

• Uhusiano na huduma za kiteknolojia

• Matangazo kwenye televisheni na redio

• Mitandao ya kijamii

Ili kufanikisha masomo ni muhimu kufahamu mchanganyiko wa mambo

yafuatayo:

• Wateja wako ni kina nani, wa aina gani, utawafikiaje, njia za usambazaji

• Mikakati yako ya uuzaji na makisio yake

• Fahamu washindani wako, waelewe na wasiwe maadui zako

• Fahamu sehemu za uzito/uwezo wao na madhaifu yao

• Wanakuzidi nini, na wapi

• Weka mikakati ya kujaza mapungufu yako

Umuhimu wa masoko

Wakati uliopita, watu walisema “Tunauza tunachozalisha” usemi huu ni sawa kwa bidhaa fulani ambazo si kila mtu anaweza kuzalisha kama vile saruji. Siku za leo biashara ndiyo inatafuta wateja wanataka nini kabla ya kuingia kwenye uzalishaji au utoaji wa huduma

Wajibu wa muuzaji

• Kutafuta masoko na matakwa yake/ mahitaji yake

• Kusimamia uzalishaji wa mazao, huduma na aina

• Kuinua bidhaa na huduma

• Kuchagua na kushawishi njia za usambazaji

• Kupata mauzo ya mazao na huduma

• Kupanga makubaliano ya uzalishaji

• Kupanga Kupanga na kuratibu shughuli zote za masoko

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 maoni juu ya “Soko la mbogamboga hutokana na uzalishaji

  1. Nimefurahi sana kukutana na jarida la mkulimambunifu leo, naomba kujulishwa namna ya kujiunga ili niweze kupata majarida kwa ajili ya kujisomea. Asante.

    1. Habari, Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuwasiliana nasi.

      Tunafurahi kusikia kuwa umependezwa na jarida letu na unahitaji kuwa miongoni mwa wasomaji na watekelezaji wa kilimo hai kupitia jarida hili. Kama una kikundi wa wakulima basi tutumia jina la kinundi chako, jina la kiongozi na namba ya simu, sanduku la posta na pia ungetueleza mnajishughulisha na nini. Tukipata mawasilianao ya simu tutakupigia.

      Kama ni wewe binafsi basi tutumie email yako yaani barua pepe ili tuweke kukutumia jarida

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *