Mboga ni mojawapo ya chakula bora kwani zikiliwa zenyewe kwa kuchanganya zina viini lishe tosha. Hata hivyo, mboga zimegawanyika katika makundi kutokana na sehemu ya mmea iliyo muhimu katika chakula cha binadamu na viini lishe vipatikanavyo. Sehemu za mmea wa mboga zinazotumika kama chakula ni pamoja na mizizi, shina, majani, matunda, maua na mbegu. Kazi muhimu za mboga kwenye chakula…
Tumia mazao funikizi kwa chakula na kulisha mifugo
Mazao funikizi siyo mageni sana kwa wakulima walio wengi isipokuwa kwa wale ambao ndio kwanza wanaanza kujiingiza katika kilimo hifadhi. Si mazao yote funikizi yanayoweza kutumika kulishia mifugo moja kwa moja mara baada ya kuvuna kutoka shambani. Mengine ni lazima yafanyiwe maandalizi fulani ndipo yatumike kulishia. Mazao funikizi kama vile, canavalia yanahitajika kukaushwa kwanza na kuandaliwa vyema kabla ya kulisha…
Chanjo ya matone ya mdondo; Kitaalamu I-2 vaccine
Chanjo hii ina virusi hai vya mdondo vinavyotengeneza kinga dhidi ya ugonjwa wa mdondo/kideri. Virusi hivi vimeoteshwa kwenye mayai ya kuku wasiokuwa na magonjwa anuwai. Chanjo hii inapatikana katika chupa zenye ujazo wa dozi ya kuku 100 na kuku 200. Hifadhi Chanjo ya 1-2 imehifadhiwa katika chupa za plastiki ambazo ni rahisi kusafirisha na zina mfuniko wenye sili. Ukishafungua mfuniko…
Raphael: Mkulima asiyeona anayeendesha maisha yake kwa kilimo
Ukimuona akiwa shambani anavyojituma huwezi kumdhania kuwa ana ulemavu wa macho. Analima bila kupumzika, na hata katika maongezi, huongea huku akiendelea na shughuli zake kama kawaida. Kuna msemo usemao,