- Kilimo
Sambaza chapisho hili

Jaffer J. Kesowani anasema: Habari Mkulima Mbunifu. Nimeona makala yako ya nyanya pori na nimeazimia kulima. Mtihani niliokutana nao ni wapi nitapata mbegu. Nikaona swali hili nilirudishe kwenu.

Mkulima Mbunifu anajibu: Mbegu za nyanya pori zinapatikana madukani kwenye maduka ya pembejeo na zinauzwa kama mbegu zingine. Mkulima anahitajika kununua kulingana na ukubwa wa shamba lake.

Nestory Mwangoka anasema: Mkulima mbunifu ni jarida zuri sana. Linaelimisha sana kwa upande wa kilimo kwani kwa sehemu ndogo tu ya shamba unaweza kulima na kujipatia mazao au mbogamboga za kula wewe na familia yako na ya ziada ukauza.

Mkulima Mbunifu anajibu: Asante sana kwa mrejesho chanya, tunaomba na wengine wasisitize waweze kujipatia elimu hii yenye manufaa kwa wakulima.

Denis Miliyo anauliza:  Nalipataje jarida la Mkulima Mbunifu?

Mkulima Mbunifu anajibu: Kwa kuwa unauwezo wa kuingia mtandaoni, unaweza ukajisomea au kupakua nakala yako kupitia tovuti yetu ya www.mkulimambunifu.org na ukapata nakala zote za kila mwezi.

Pia, kama una kikundi cha kilimo, unaweza ukatutumia taarifa za kikundi chako ikiwa ni jina la kikundi, anuani ya posta, idadi ya wanakikundi, jina la kiongozi na namba yake ya simu ili tukipata nyongeza ya nakala hapo baadaye tuweze kuwatumia. Karibu sana Mkulima Mbunifu

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *