Ni muhimu kuzingatia utunzaji wa vifaranga

Kwa karne na miaka mingi, ufugaji wa kuku imekuwa ni kazi muhimu na inayokubalika katika jamii nyingi. Ni kazi isiyohitaji gharama kubwa sana, ambayo imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwa wanaiofanya kibiashara. Tatizo ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa wafugaji walio wengi, ni kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia siku ya kwanza wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa. Hali hii imekuwa ikiwasababishia wafugaji hasara na kuwakatisha tamaa.

Hii inatokana na wafugaji kuzingatia kuwa na banda na chakula tu, bila kuzingatia aina nyingine ya matunzo muhimu yanayohitajika kwa ajili ya kuwafanya vifaranga waishi na kukua wakiwa na afya. Haya ni baadhi ya mambo muhimu kuanzia siku ya kwanza ili vifaranga wako wasipate madhara na hatimaye kufa:

• Mara baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe sehemu yenye joto kwa wastani unaohitajika. 

• Hakikisha sehemu ya banda ulipowaweka vifaranga ni kavu, na isiyokuwa na vimelea.

• Hakikisha vifaranga wote wanapata chanjo ya mahepe (mareks) siku ya kwanza.

• Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa kideri.

• Inapofika siku ya 14, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa gumboro. • Rudia chanjo ya kideri katika siku ya ishirini na moja.

• Siku ya ishirini na nane, rudia tena chanjo ya gumboro • Baada ya wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga wako wanapata chanjo ya ndui.

Kwa kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na uhakika kuwa kuku wako ni salama. Watakuwa bila tatizo, jambo ambalo litakupa uhakika wa kuwa na mazao bora, na hatimaye kupata faida. Pamoja na hayo, hakikisha kuwa unazingatia lishe bora. Hii itasaidia kuwapa kuku afya njema na kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa.

**Kamwe usiwape kuku vyakula vilivyooza. Hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa kuku na kusababishia hasara.

Maoni

Ni kweli kule vifaranga ni kazi kubwa sana na ukiweza kuzuia vifo vya vifaranga basi utakuwa umemaliza kazi, vifo vingi sana ni wakati wa vifaranga.

Na usafi ni muhimu sana hasa kuwakinga na ugonjwa wa kuhara Damu ambao nao huwamaliza kabisa vifaranga na ni bora vile vile wakapewa dawa ya kuzuia kuhara damu kama vile Amprolium ni dawa nzuri sana, na wanatakiwa wapewe hata kama hawaumwi.

Nawapongeza kwa ushauri wenu.naomba mnieleweshe ugonjwa wa mahepe.dalili na kinga yake

Nina vifaranga wa kisasa wa mayai wenye umri wa miezi mitatu 3 naomba kufahamu mambo haya:- je? kuna athari nikiwapa maji bila kuweka vitamini mfano vitalyte,vitastress
pia kuna madhara gani wakila pumba labda kwa mda wa siku 3 pindi ambacho lishe inakuwa imeisha nikiwa naandaa nyingine

mkuu kwa hao pure kisasa ni makosa makubwa sana kwapatia pumba wakati chakul;a kimeisha, yaani usfanye huo mchezo kabisa wanatakwia kuendela na ratiba yao ya msosi na hata kubadili kutoka grower kwenda layer waga kuna hatua sasa ukiwapa pumba ni kuwatesa.

Kuhusu kuto kuwapa Vitamini haina shida si lazima daily wapewe vitamin, mara zimngine wapewe maji pekee vitamin ni mara moja moja tena kipindi cha chanjo au kama wanaumwa

nilipenda somo jinsi yakuweza kukabiliana vifo vya vifaranga ...wafugaji wengi tumekuwa tukifurahi pale vifaranga vikotolewa bila kuchukua tahadhari namna ya kuwa kinga na ma magonjwa nyemelezi...

nimelipenda somo jinsi yakuweza kukabiliana vifo vya vifaranga ...wafugaji wengi tumekuwa tukifurahi pale vifaranga vikotolewa bila kuchukua tahadhari namna ya kuwa kinga na magonjwa nyemelezi...

nahitaji baanda la ukubwa gani kufuga kuku elfu mbili wa kienyeji?

Jamani wajasiriamali hongereni na majukumu,napenda kuwataarifu kwamba Molinda Poultry imeleta mbegu mpya ya kuku,vifaranga wataanza kupatikana juma la pili mwezi Aprili.Ni kuku wenye uzito mkubwa wastani wa kilo sita mpaka saba.Kuku hawa wanaitwa new southern Hemshire utagaji ni wastani wa mayai 282 kwa mwaka.Mimi napatikana Arusha.Kwa mawasiliano piga simu namba 0754 917085

Mnapatikana Arusha sehemu gani na kuku mnauzaja?

Tupo Sakina kibanda cha maziwa karibu sana.

Nataka kufuga kanga nyeupe kama uko nazo nipigie simu niko Nairobi Kenya (+254) 0729795208

HABARI NJEMA.
-Kuwa wa kwanza kupata Kuku aina ya KARI kutoka Kenya ni Kuku wa Kienyeji wenye utagaji mkubwa kuliko kuku wa kisasa wa mayai, hawa kuku ni I proved kienyeji wenye uwezo mkubwa na wa kipekee katika utagaji na wanapatikana kwa Oda, Vifaranga wanao patikana ni wa wiki moja.

Phone 0783-69-10-72

Ndugu wafugaji habari za leo,leo nataka kutoa angalizo kuhusu utoaji chanjo ya kideri na gumboro.Wengi wetu tumekua tukiwapa kuku chanjo ya kideri bila kufuata maelekezo vizuri,tumekua tukitumia maji ya bomba kuchanyia dawa bila kufahamu kwamba maji hayo yanakuwa na dawa ambayo inaua vijidudu vilivyomo kwenya chanjo ya newcastle matokeo yake ni kuku kupata kideri.Hivyo tunashauriwa kutumia maziwa yalitolewa mafuta na kuchanganya na maji yaliochemshwa na kupoa

Tunapenda kuwataarifu kuwa kampuni ya KUKU KLKUA iliyopo mkoa wa Kilimanjaro inatoa kwa mkopo vifaranga,chakula,madawa na chanjo kwa wanavikundi kila mmoja anapata vifaranga mia moja. Mkopo huu unarudishwa baada ya kuku wakianza kutaga na kuuza mayai. Kwa taarifa zaidi piga 0718 503 330 AU 0766 503 330. Karibuni woooote

nipe fomula ya kulisha kuku 1 wa w10 na kuendelea au kuku mmoja anakula kiasi gani cha chakula kwa siku

ningependa kujua jinsi ya ufugaji kuku wa kienyeji,banda lake liweje na jinsi ya kuwalisha kama sitataka kufuga kiasili kwa kuwafungulia asubuhi na jioni kuwafungia,tayari nimeanza na kuku jike wanne na jogoo mmoja ila hawa majike utagaji wao sio mzuri wanataga mayai machache kuanzia matano hadi saba. hivyo ningomba kuelekezwa jinsi ya ufugaji wa kisasa wa kuku wa kienyejii,naamini hadi mwakani nitakuwa naanza kujiongezea kipato kutokana na kuku haooo

Kwa Kuku wa Kienyeji hata uwafuge vipi hawawezi kutaga zaidi ya uwezo wao,

Ni kweli kabisa kuku hao ni wengi na wanatosha kwa kuanzia
Ifikapo mwakani ni kuku wengi nitumiea email yako upate soft copy ya kitabu ujifunze zaid kwenye namba 0655390755

Naomba nami unitumie hiyo soft kopi.

Nashukuru kwa elimu yenu nzuri.Nahitaji vifaranga wa KARI nipo Mbeya mjini.Naweza kupata hao vifaranga?

Ya unaweza pata ila maswala ya kuwasafirisha ni juu yako

naombeni msaada wenu ndugu zangu nina ndoto za kufuga kuku ila kipato ndo kinanisumbua kama kuna sehemu ya kuweza kukopeshwa mnijulishe nawategemea sana!!!

Mkuu wewe anza na kile ulicho nacho, unaweza anza hata na kuku mmoja na ukawa unaishi naye ndani hapo hapo unapo lala wewe, safari huanza kwa kupiga hatu moja mbele, wewe anza na ulicho nacho

ndugunashukuruni sana kwa maoni, nami nimfugaji mdogo nina kuku kama sitini(60) wa kienyeji. kaka chasha ninahitaji hivyo vifaranga toka kenya(KARI) nitavipataje na ni shilingi ngapi? ninafuga moshi ila mimi naishi arusha. simu 0758265356

Mkuu nitafute kwa 0767 69 10 71 niko Arusha na Karatu tuna vifaranga Bora kabisa wa Kuroiler kutoka India hawa waliletwa Uganda.

jamani hebu nijuzeni kuhusu chanjo ya mahepe, ni dalili zake

Kwenye mtandao soma jarida la Mkulima Mbunifu toleo la 26 Novemba, 2014 ukurasa wa 5

nahitaji vifaranga hao aina ya KARI kutoka kenya nipo dsm na je unauzaje pia wakikua wana uwezo wa kuatamia mayai

Mkuu hawaatamii wanataga tu, Dar unawapa kwa Oda mkuu

Admin uwe unajaribu kupitia post zaina potosha na kuzifuta humu, kuna upotoshaji mkubwa sana unafanyika vinginevyo hii site itakuwa nayo ni ya kihuni tu

Sawa, tutafuatilia. Asante kwa ushauri

Kwa sasa inaweza pata Mashine za Kuangulia kutoka Kwetu, na Dis asemble kwamba tunaweza kuja kukuunganishia huko uliko ili kupunguza gharama za Usafiri.
pia unaweza pata spare zote za incubator na pia tunatoa matengenezo ya incubator zilizo haribika.
1. Mayai 88 Tsh 800000

2. Mayai 176 Tsh 1, 100,000

3. mayai 264 Tsh 1, 200,000

4. Mayai 352 Tsh 1, 400,000

5. Mayai 440 Tsh 1,600,000

6.Mayai 528 Tsh 1,700,000
7.Mayai 616 Tsh 1,800,000

8. Mayai 704 Tsh 1,900,000

9. Mayai 880 Tsh 2,000,000

10. Mayai 1056 Tsh 2, 300,000

11. Mayai 1232 Tsh 2,600,000

tuko Arusha na tunaweza kuja kuunganisha hapo ulipo, pia elimu ya ufugaji kibiashara inatolewa ikiwa ni pamoja na vifaranga.

0767 691071

Tatizo bwana chacha umekuwa na maneno mengi sana ambayo hayana ukweli

Asante kwa taarifa

Kaka Abel nahitaji hiyo machine naomba unitafute facebook jina hlo hapo. Asante!

Naamini amepata ujumbe na atakutafuta

Naitwa ABEL SENG’ONGO.Nauza na kusambaza AUTOMATIC COMPUTERIZED INCUBATOR za Kisasa Kutoka JAPANI na zenye uwezo wa kutumia SOLA,GENERATOR na UMEME,Kuanzia mayai 60,100,170,500,1000,2000,4000,6000,8000 hadi 10,000 au kulingana na mahitaji yako.ZINATUMIA SYSTEM YA KOMPYUTA KUGEUZA MAYAI,KUONGEZA NA KUPUNGUZA JOTO,KUONGEZA NA KUPUNGUZA UNYEVUNYEVU,INACONTROL OKSIJENI INAYOTAKIWA.
:MAYAI :BEI
Mayai-528— bei-2,000,000/=
Mayai-1056—bei- 3,500,000/=
Mayai-8448 –bei-12,000,000/=
mayai-48—- bei-400,000/=
Mayai-96—bei- 500,000/=
MASHINE YA KUNYONYOLEA KUKU MMOJA KWA SEKUNDE 10 NI 1,500,000/=
WASILIANA NAMI KWA 0765313355 au 0788384285 au 0653557474 E-mail [email protected]
UTALETEWA MPAKA MLANGONI
Zina vipimo maalumu kwa yai la kila aina kama kuku,bata,batamzinga,mbuni,kwale,njiwa,kanga,kenge,nyoka nk
SPEA UTAPEWA BUREE

Asante kwa taarifa

Asante kwa taarifa

KUHUSU VIFARANGA

Habari za shughuri wakuu? Kuna mambo ningependa kuyaweka wazi ili watu wayajue hasa sawa la Vifaranga na jinsi ya kuwapata.

1. VIFARANGA
Vifaranga wanapatikana kwa kuweka Oda na si vinginevyo, ni vigumu sana kufanyia kazi oda ya mtu ambayo haiko open, hivyo ni mpaka uweke oda ndo nikuweke kwenye rist na si vinginevyo.

2. TRASNSPORT
Usafiri kwa watu wa mbali ni juu yako wewe mwenyewe mimi naweza saidia kuwapakia kwenye gari ila usalama wao wakiwa njiani hautakuwa juu yangu tena kwa nmna yoyote ile.

3. WALIOKO MIKOA YA MBALI
Kwa wlio mbali kwa kweli nisikudanganye kwamba naweza tuma voifaranga mfano KIGOMA, KAGERA, TABORA, MBEYA, SUMBAWANGA, RUKWA NA KAZALIKA.
Huko ni mbali sana na hata hao vifaranga tutakuwa tunawatesa sana HIVYO HUKO KWA KWELI LABDA UJE UWACHUKUE MWENYEWE KWA SABABU KUNA MTU ALISHA WAHI KUTOKA SUMBAWANGA AKAJA KUWAFUATA ARUSHA MWENYEWE.

Kuna kampuni za Ndege kama Precision Air walikuwaga na Ndege yenye kuweza kubeba viumbe hai, ilikuwa ni rahisi sana kutuma vifaranga Mwanza, Bukoba au Kigoma au Mtwara ila kwa sasa hawana tena hiyo ndege hivyo inakuwa vigumu sana.

KWA HUKO KWA BAADAE MWAKANI NITAANZA KUUZA MAYAI YA KUTOTOLESHA AMBAPO MTU ATAANGUA MWENYEWE HUKO, NA MAYAI YATAPATIKANA KWA UPENDELEO PEKEE KWA WATU WA MBALI.

MWISHO: CHASHA POULTRY FARM sio mfanya kazi wa Mkulima mbunifu na mimi humu ndani ni member tu hivyo msawala ya kama Manual yanawahusu wahusika mimi niliyo yano ni ya kwangu binafisi niliyo develop mwenyewe.

Mawasiliano [email protected], 0767-69-10-71

Ahsanten kwa ushauri wenu. Nipo mkoani Iringa nauliza kama naweza pata vifaranga wa KARI!
Pia naombeni kutumiwa Soft copy yenye mwongozo wa kufuga kuku. E-mail yangu:[email protected]

Asante, Nitakutumia

Unapenda kufuga kuku wa kienyeji????
Mradi wa KUKU KUKUA unatoa kwa mkopo vifaranga mia moja, chakula na madawa na chanjo kwa kipindi chote cha ufugaji na soko la mayai au vifaranga. Shamba letu lipo Bomang'ombe, wilaya ya Hai, Kilimanjaro.

Wasiliana nasi kwa: 0718503330 au 0766503330. Email [email protected], Tovuti: www.kuku-kukua.org

Asante kwa taarifa

Habari za leo, nipo Zanzibar, tafadhali naomba soft copy ya ufugaji wa kuku kuroiler, kware na kanga.
Ni mategemeo yangu ntajibiwa baada ya muda mfupi.

Kwasasa hatuna taarifa kamili kuhusiana na ndege hao ila zikishachapishwa utazipata

kaka chacha hizo incubator safi sana!

Niwapongeze kwa tovuti maridhawa imejaa mafunzo mengi.
Lakini pia nisikitike kwa kugeuzwa uwanja huu kama duka la incubators na mambo mengine ya ufugaji.
Sielewimatangazo hayo kama ni yenu ama ni yetu wasomaji!
Nilichogundua ni kitu kimoja kikubwa na kibaya sana, naamininsote tufugao ni watu tulioamua kukuza kipato chetu, sasa iweje wajasiriamali kuuziana vifaa kwa bei ghali mno? hizi.incubagor mazouza kwa karibu mara 10ya bei yake ya kiwandaniivi.kweli wen,etu mna upendo nasi ama ni njia ya kutuibia kwa tusiojua
Nisameheni kama nimewakwaza lamini sijapenda hii hali.iliyojitokeza!
Kama .nmwogopa mungu mliouza incubators kwa bei za ajbu warudishieni watu.pesa.mliyokwapha!

Beiya incubator nilihoagiza mimi.kutoka huko.huko mnakotoa nyie ya mayai 528 ni shs 980,000 ikiwa tayariiko Dar!

Nyie wenzetu mna incubator zinazotaga mayai zenyewe

Nashukuru kwa taarifa, jaribu kupunguza ukali wa maneno

Tafadhali naomba maelezo juu ya incubator uliyosema, ili nami niagize.

Au tuwasiliane kwa email [email protected]

Pages

Andika maoni mpya

Plain text

  • Hakuna vishikizo vya HTML vinavyokubaliwa
  • Anuani ya ukurasa kwenye mtandano na anwani za barua pepe hubadilika kuwa viungo moja kwa moja.
  • Mistari na aya zinajipanga zenyewe.