- Kilimo

Epuka haya ili usipate hasara katika kilimo

Sambaza chapisho hili

Kwa siku za nyuma, takwimu zilionesha kuwa 80% ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo jambo ambalo kwa sasa inaonekana idadi yao kupungua na kufikia 60%. Hii huenda ikawa ni kutokana na hasara zinazopatikana kwenye kilimo.

Hasara katika kilimo zimekuwa ni jambo kubwa ambalo linasumbua vichwa vya wakulima wengi ndani na nje ya Tanzania. Hasara hizi huweza kusababishwa na mambo mengi sana lakini leo tutajifunza mambo machache.

Usimamizi mbaya

Kuna mambo mengi sana ambayo mkulima au anayejishughulisha na kilimo anatakiwa kuwa nayo makini. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuwa makini katika usimamizi wa mazao au mifugo anayotaka au anayoifuga.

Katika miaka ya karibuni kumeibuka wimbi la watu kujiingiza katika kilimo cha mazao au ufugaji kwa namna ambayo imewafanya wajutie kulima au kufuga.

Hii inatokana na wengi wao kwa namna moja au nyingine kupata hasara ya hali ya juu na wengine kupoteza makazi, mashamba au mali ambazo walikuwa wanazimiliki kwa sababu ya mikopo waliyoichukua.

Wengi wa wakulima wamejiingiza katika kilimo huku wakiwa na muda mchache wa kuangalia miradi walioianzisha na hivyo kuishia kufanya kilimo kwa njia ya simu. Hii imewagharimu wengi na hata kupelekea wengine kuishia kulia na kulaani kilimo kuwa si kitu/biashara ya kufanya. Lakini tatizo kubwa ni usimamizi mbovu wa miradi.

Ushauri: Usianze kilimo kama huna uhakika na usimamizi wako au uangalizi wa karibu wa mradi wako wa kilimo.

Mkulima mzuri anajua kujipanga vyema kabla ya kuanza kufanya shughuli za kilimo

Kutokuwa na taarifa za uhakika

Katika kilimo taarifa ni kitu mhimu sana kwa maendeleo na ufaulu wa mradi wako unaotaka kuufanya.

Taarifa zinazo hitajika ni pamoja na:

  • Eneo sahihi kwa mradi mfano, aina ya zao kwa eneo sahihi.
  • Namna ya kuendesha mradi, mfano, unazalishaje mazao au mifugo.
  • Changamoto za mradi.
  • Soko na usafirishaji.n.k.

Ushauri: Fahamu ni nini uzalishe, wapi, lini, kwanini na uuze wapi.

Hali ya hewa

Hali ya hewa mara nyingi si rahisi kuweza kuidhibiti, lakini unaweza ukapunguza uwezekano wa kupunguza hasara.

Ukizingatia hayo kwa umakini na kuongeza ubunifu wa ziada, ni hakika kuwa utaepuka hasara zisizokuwa za lazima.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 maoni juu ya “Epuka haya ili usipate hasara katika kilimo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *